Tulonge

Asali mbichi imekuwa ikitumika kama dawa na mataifa kwa matatizo mbalimbali kuanzia kwenye kikohozi hadi vidodnda vya moto.

 

Mdau asali unaitumia kwa matatizo gani? Mie natumia asali mbichi kuchanganyia tangawizi na limao ajili ya kikohozi. Pia asali mbichi peke yake huwa nawapaka watoto kwenye michubuko/viji-jeraha wanayopata kwenye michezo.

Ukweni kwangu sana sana wanachanganya asali na unga wa mdalasini (Cinnamon), viungo tutumiavyo kwenye pilau ajili ya kupunguza Blood Cholesterol Levels, kupunguza maumivu ya Arthrities, kuumwa jino, kuvumbiwa na pia ajili ya kikohozi na flu kwa ujumla. Pia asali tupu yatumika kwenye mwili (ngozi) kuondoa vijipele na ngozi inakuwa laini nyororo hivyo kuifanya asali kuwa mkorogo wa asili kwa wale wapenda mikorogo.

 

Je wewe unaitumia vipi? Naomba tubadirishane mawazo na wengine tufaidike zaidi na matumizi ya asali.

Views: 4305

Replies to This Discussion

Asanteeeeeeeeeeeeeeeee mi nitaitumia kwa vidonda vya tumbo. sikuwa najua hilo, asante ma mkubwa.

asali ni nzuri kwa vidonda vya tumbo tumbo kujaa gesi kiungulia na kuungua kwa moto, unatumia kupaka sehemu yenye jelaha, na hata kutumia kwa afya unatumia kupaka kwenye mkate kama jam,

Asante kwa elimu hii Mama, mengine ndo kwanza nimeyaona hapa

Asante sana Bonielly, kuanzia leo naanza tumia kwenye mkate.
Dismas... Hata mie nimejifunza mengi kwa wakwe zangu wazungu

mimi pia huwa natumia kwa kuchanganya na magadi soda kwaajili ya mafua, pia huwa nachanganya na tangawizi, limao na magadi ya kawaida kwa ajili ya kifua kinachobana.inasaidia sana kwa kweli.

pia waweza kuchanganya asali na vitunguu swaumu ukatumia kama stimining ya nywele kwa wale wa dada wenye tatizo la kukatika katika nywele.

Asante mkwe, mama manka. Kumbe hata nywele inafaa, safi sana

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*