Tulonge

MAPEMA wiki iliyopita, ilitawala habari ya tunda la stafeli kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa hatari, ukiwemo ugonjwa wa saratani. Hata hivyo, utafiti wa kwanza kuonesha uwezo wa stafeli kutibu saratani, uligundulika tangu miaka ya sabini, lakini ulifanywa siri hadi hivi karibuni ulipowekwa bayana tena.

Hivi sasa wakereketwa wa tiba mbadala na dunia kwa ujumla, wanafahamu kuwa stafeli lina virutubisho vyenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya saratani kushinda hata dawa za kisasa. Tunda hili linapatikana nchini kwa wingi, mjini na vijijini. Kwa lugha za kigeni linajulikana pia kama Soursop au Graviola.

VIRUTUBISHO VILIVYOMO
Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, stafeli limesheheni idadi kubwa ya virutubisho ambavyo ni: Amino Acid, Acetogenins, Vitamin C, Iron, Riboflavin, Phosphorus, Thiamine, Calcium, Carbohydrates, Niacin na Fibers na vingine vingi.

SARATANI NA STAFELI
Ingawa suala la stafeli peke yake kutibu saratani lina mjadala, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani. Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa wagonjwa wa saratani njia nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya mionzi na kupata ahueni kubwa.

USHAHIDI WA KIMAABARA
Zaidi ya majaribio 20 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:
Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.
Stafeli lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika kutibu aina mbalimbali ya saratani.

Mchanganyiko wa virutubisho vya ‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huua seli (cells) zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.
Stafeli hudhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.

UMUHIMU WA STAFELI KWA WANAOTUMIA TIBA YA KISASA
Mgonjwa wa saratani anayetumia tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana stafeli kwani lenyewe husaidia kupunguza makali ya dawa anazotumia.

Views: 1157

Replies to This Discussion

Asante kwa Elimu hii. Sikumbuki mara ya mwinsho kula tunda hili ni lini... ni zamani sana!!! Itabidi nalenyewe niliweke kwenye list!!!

Asante sana ku-share nasi. Nilisikia kwenye BBC nafikiri ni mwaka jana ingawa wanasema uchunguzi unaendelea. Ni habari njema kwetu na habari mbaya kwa greedy Pharmaceutical Industry kwani dawa ya cancer ikipatikana watafilis
Pharmaceutical Industry itafilisika. Nitaupanda mti wa tunda hili kwenye bustani yangu Mbweni & Tegeta

Ahsante sana ; kwa kweli itabidi kulitafuta stafeli kwa kila njia lli liwe sehemu ya mlo

dah mwanangu anakula sana hili tunda kiukweli huwa namshangaaga kwani mimi sipendi kabisa tangu nimle funza sina hamu. nyumbani yapo ila kwa sasa msimu haupo had badaye. mama Malaika ukija msimu wake inabidi nikuwekee kigoda chini ya mti na kaka akupandie juu kukutungulia.

We  Angela rekebisah na utengue kauli... Yani Kaka yako ampandie juu Mama kumtungulia na yeye akae tu kwenye kigoda chini ?

Uko ulipokuwa umejificha pamekuharibu... tehehehehee..

ANGELA JULIUS said:

kweli Dixson akili yako imetenguka sijui na ile milio ya silaha manake unachonieleza umekiunda kwelikweli, ila naimani mama Malaika atanielewa tuu hata Bonielly angenielewa pia.

asante kwa ufahamisho, lakini sikumbuki nilikula lini hili tunda.

Ha haa haa haa haa haaa.... Dixon

Dixon Kaishozi said:

We  Angela rekebisah na utengue kauli... Yani Kaka yako ampandie juu Mama kumtungulia na yeye akae tu kwenye kigoda chini ?

Uko ulipokuwa umejificha pamekuharibu... tehehehehee..

ANGELA JULIUS said:

dah mwanangu anakula sana hili tunda kiukweli huwa namshangaaga kwani mimi sipendi kabisa tangu nimle funza sina hamu. nyumbani yapo ila kwa sasa msimu haupo had badaye. mama Malaika ukija msimu wake inabidi nikuwekee kigoda chini ya mti na kaka akupandie juu kukutungulia.

Angela nimekuelewa uzuri. Nitakuja nipatae matunda, na hata kama kaka yako hayupo nitapanda mwenyewe huko mtini kwani bado napanda mitini kwenye camping. LOL...
 
ANGELA JULIUS said:

kweli Dixson akili yako imetenguka sijui na ile milio ya silaha manake unachonieleza umekiunda kwelikweli, ila naimani mama Malaika atanielewa tuu hata Bonielly angenielewa pia.

Hahahahahaah Angela milio ya silaha gani?

ANGELA JULIUS said:

kweli Dixson akili yako imetenguka sijui na ile milio ya silaha manake unachonieleza umekiunda kwelikweli, ila naimani mama Malaika atanielewa tuu hata Bonielly angenielewa pia.

ha ha ha ha Lucie angalia kwenye picha alizoupdate utaona alienda camp moja hv mahali fulani huko alachuga lol

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*