Tulonge

  Assallam Allaykum ya hikhwatu fi Llah!

Baada ya kuangalia mada ya msingi leo naomba nitoe kwa uchache maana ya Shahada nanyi mchangie humo.

Shahada kwa minajiri ya dini ya kiislamu ni kushuhudia kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa Hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhhammadi (S.A.W) ni mja na mtume wake.

Hivyo basi ili shahada iweze kutia inatakikana kuwe na vitu vitatu vya msingi ambavyo ni ;

(1)kukubali katika moyo

(2)kutamka kwa ulimi

(3)kuweka katika vitendo hayo unayoyaitakidi.

Na katika hili msidhani kuwa limetokea katika zama hizi za Mtume wa Mwisho yaani Mohhammad(S.A.W) bali ilikuwa ni amri ya Allah Kwa mitume wot e aliowatuma.Kwa mfano katika Biblia YOHANA MT. 17:3 Yesu anasema, Na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe,Mungu wa pekee na wa kweli na yesu kristo uliyemtuma.

Kwa haya machache yanatosha kwa leo naomba mnijuze zaidi katika haya niliyonayo.

Wabbillah tawfiq Assallam Allaykum warhammatullah wabbarrakatuh!

Views: 840

Replies to This Discussion

swadata ndugu riziki huwezi kuwa mwislamu bila ya kupiga shahada na ni nguzo ya kwanza katika uisamu na kila mwislamu yampasa kusema shahada kabla kutoka nyumbani kwako na unapolala pia watakikana useme shahada nasema mola akujzi kheri na baraka zake zikushukie kaka ili tupe elmu ya dini mola atulinde na shari na atupe ya kheri
Amin! kaka nashukuru kwa mchango wako Allah atuzidishie elmu sote insha-Allah
Inshaallah, Mwenyezi Mungu atufishe tungali tunatamka shahada!

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*