Share 'Edward Lowassa VS John Magufuli Nani Zaidi?'
Kila baada ya miaka mitano, Tanzania na Watanzania hupata nafasi ya kumchagua kiongozi wa ngazi ya juu kabisa yaani Rais. Utaratibu huo ni wa kikatiba, na kila Mtanzania hana budi kushiriki zoezi hilo ili kumpata kiongozi huyo wa nchi. Kwa sasa ni wazi kabisa kuwa, viongozi wenye nguvu katika nafasi hiyo ni wawili tu kwa Tanzania bara, yaani Edward Lowassa wa CHADEMA anayewakilisha UKAWA, na John Pombe Magufuli wa CCM. Wewe kama mpiga kura, unadhani ni nani atafaa kuwa kiongozi wa nchi hii kati ya Edward Lowassa--CHADEMA na John Pombe Magufuli--CCM.?