Tulonge

Kila baada ya miaka mitano, Tanzania na Watanzania hupata nafasi ya kumchagua kiongozi wa ngazi ya juu kabisa yaani Rais. Utaratibu huo ni wa kikatiba, na kila Mtanzania hana budi kushiriki zoezi hilo ili kumpata kiongozi huyo wa nchi. Kwa sasa ni wazi kabisa kuwa, viongozi wenye nguvu katika nafasi hiyo ni wawili tu kwa Tanzania bara, yaani Edward Lowassa wa CHADEMA anayewakilisha UKAWA, na John Pombe Magufuli wa CCM. Wewe kama mpiga kura, unadhani ni nani atafaa kuwa kiongozi wa nchi hii kati ya Edward Lowassa--CHADEMA na John Pombe Magufuli--CCM.?

Views: 523

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by eddie on August 23, 2016 at 23:32

Nilikuwa busy sana...sikuweza kujibu on time. Huku kwema tu Dada Mama Malaika!

Magufuli is My President. Nakwambia dada Magufuli amenifurahisha sana...maana miaka mitatu nilikuwa nasubiri waje jamaa wa ubalozi waje kuchukua finger print kwa ajili ya passport yangu...baada ya Magufuli kuingia madarakani haikuchukua week walinitafuta..na within 2 weeks walinitumia passport yangu....yaani najiuliza kwanini uzembe ulitapakaa hivi??

Comment by Mama Malaika on March 16, 2016 at 0:07
Hapa kazi tu @ kaka Eddie.
Kwema sijui pande hiyo. Naona CHA kaadimika sana maana kasi ya Magufuli si mchezo, kazi ni kazi matumaini peleka Monduli. Teh teh teh......
Comment by eddie on November 15, 2015 at 22:15

Kwema humu lakini??

Comment by Mama Malaika on November 11, 2015 at 2:22
CHA the Optmist... mbona kimya sana au bado haujarudi toka kwenye campaign za Luwasa??
Comment by eddie on November 7, 2015 at 10:45

Hapa kazi tu!

Comment by Mama Malaika on September 2, 2015 at 9:38
CHA the Optimist.... Msimamo wangu uko pale pale. Mtu anayejinadi iwapo atavhaguliwa uraisi atawaondoa watanzania kwenye umasikinu wakati huko kwao hajapafanya mfano watu wanataabika hata maji hakuna na huyo ni mbunge wa miaka mingi tokea CHA the Optimist ulipokuwa mtoto wa Primary School. Teh teh teh....
Comment by CHA the Optimist on August 29, 2015 at 23:00

Mama M, in response to your statement, ni kwamba; makada mbalimbali akiwemo Mzee Kingunge Ngombare wamelalamika kuwa, uteuzi wa jina la mgombea kiti cha Urais kule Dodoma haukuwa wa haki ndani ya CCM. To put it in a nutshell, Mwenyekiti wa CCM ambaye kwa sasa ni Kikwete alikuwa na majina yake teyari mfukoni. Lowassa amelalamika kuwa CCM ya sasa si ile ya Nyerere, CCM ya sasa ni ya kibabe, kanuni zao wenyewe zinakiukwa mchana kweupe. Hicho ndicho kilichomfanya Lowassa ajiondoe huko CCM. Kuhusu kukubali kugombea kupitia CHADEMA, ni kwamba kwa kanuni na taratibu za CHADEMA, hakuna mgeni wala mwenyeji katika chama hicho. Mtu ukiwa na sifa za kutosha zinazokidhi viwango vinavyotakiwa, basi unaweza kugombea nafasi yoyote. Ndiyo maana hata huyu CHA the Optimist, siku fulani miaka mitano baadaye, God willing, atarudi Rukwa kugombea Ubunge ili awaokoe ndugu zake, na hata Malaika na Denzil wakitembelea huko Rukwa wakute barabara nzuri, upatikanaji wa maji safi na salama throughout the year.

Labda niseme kwa nini nataka Lowassa awe Rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzania, na kwa nini nitampigia kura. Nitampigia kura Lowassa kwa sababu yupo katika mfumo mpya/tofauti ambao nina imani lazima aufuate ili kuweza kupiga hatua. Na hii ni kwa sababu, kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, au kwa zaidi ya nusu karne, tumekuwa na CCM iliyotokana na ASP na TANU, lakini hatua za kimaendeleo haziendani na rasilimali tulizonazo, na wala hatua za kimaendeleo haziendani na umri wa UHURU wa nchi hii wa tangu mwaka 1961.

Mama M, Tanzania ndiyo nchi pekee iliyo na mlima mrefu barani Afrika, ndiyo nchi pekee duniani kuwa na madini ya Tanzanite,  ina mbuga za wanyama, ina hifadhi za wanyama, ina watu walio na nguvu ya kufanya kazi, lakini angalia maisha ya Kitanzania au maisha ya Mtanzania, Yanasikitisha! Kwa maisha tuliyonayo au jinsi yalivyo magumu wakati tuna utajiri wa kila aina, si sawa kuwa na ufukura huu. In my opinion, CCM ambayo imekuwa ikiunda serikali tangu UHURU ndiyo tatizo. na kama CCM ndiyo imekuwa tatizo, basi hatuna budi kuiondoa ili tujaribu wengine tuone nini watafanya.

Namalizia kwa kusema 'Mpigie Kura Lowassa'

Comment by Mama Malaika on August 24, 2015 at 17:38
CHA the Optimist... nimeshangazwa sana na kitendo cha mtu kuhama chama chake kipindi cha majeruhi kisa hakupitishwa kusimama kuwa mgombea uraisi. Halafu mtu huyo huyo anahamia chama kingine na anakubali kwa moyo wote bila aibu kusimama kuwa mgombea... Hiyo ni tabia ya ULAFI na UFISI, na mtu wa hivyo sitomuamini, ana uchu wa madaraka. Natamani Mwalimu Nyerere angekuwa yuko hoi...
Comment by Mama Malaika on August 24, 2015 at 15:32
CHA the Optimist....... Kura yangu Ilikuwa nimpe Dr Slaa ya uraisi, na ya ubunge bi mdogo wa CHADEMA pale jimboni Kawe. Baada ya Dr Slaa kutosimama ugombea uraisi nimeamua kumpa Magufuli wa CCM.
Juzi nilikuwa naongea na wafanyabiashara watano toka Asia (China & India), wanasema wana hofu dhidi ya Magufuli, na wanafatilia uchaguzi wa Tanzania kwa karibu zaidi. As a global citizen, I keep my ears and eyes wide open.
Comment by Dunda on August 20, 2015 at 20:43

Kura yangu itakwenda kwa John Pombe Magufuli ndie anaefaa baada ya kuondoka kwa Mzee wangu Dr Slaa..

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*