Tulonge

Kila baada ya miaka mitano, Tanzania na Watanzania hupata nafasi ya kumchagua kiongozi wa ngazi ya juu kabisa yaani Rais. Utaratibu huo ni wa kikatiba, na kila Mtanzania hana budi kushiriki zoezi hilo ili kumpata kiongozi huyo wa nchi. Kwa sasa ni wazi kabisa kuwa, viongozi wenye nguvu katika nafasi hiyo ni wawili tu kwa Tanzania bara, yaani Edward Lowassa wa CHADEMA anayewakilisha UKAWA, na John Pombe Magufuli wa CCM. Wewe kama mpiga kura, unadhani ni nani atafaa kuwa kiongozi wa nchi hii kati ya Edward Lowassa--CHADEMA na John Pombe Magufuli--CCM.?

Views: 523

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on August 20, 2015 at 20:09

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Ujanja Ujanja.............Mama Malaika!! Ila Lowassa naye ana records zake nzuri tu. Ila kubwa zaidi ni kwamba kwa sasa hapa Tanzania, kama ulivyosema watu hawachagui chama (huko ndiko wamefikia). Ila pamoja na kutokuchagua chama, wengi wa Watanzania kwa sasa hasa vijana, wameapa kutokuirejesha CCM madarakani kupitia Magufuli. Hii inatokana na historia ndefu ya chama hicho kutokuzingatia kero za wananchi, kufumbia uozo ambao umekuwa ukitokea chini ya utawala wa CCM. Mi binafsi, ni muathirika mkubwa wa hii CCM. Hivyo basi na mimi ni moja wa watu ambao kutoka ndani ya moyo wangu, sintompigia kura huyu Magufuli kwa maana naamini hatakuwa na jipya. Bora tuangalie upande wa pili.

Comment by Mama Malaika on August 20, 2015 at 2:22
Mie siko ajili ya chama au ushabiki, kura yangu natoa kwa mtu hivyo nampa huyo John Pombe Magufuli. Huyu Luwasa alikuwa Premier few years ago sikuona chochote zaidi ya ujanja ujanja tu.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*