Tulonge

Kila walipoenda walitumia njia hii ili watawale wapate kuiba. Na bado wanaendelea....

Views: 217

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 18, 2014 at 10:57
Dixon... Hakuna faida inayopatikana zaidi zaidi ni uchafu wa mazingira (taka za sumu ardhini, kwenye vyanzo vya maji na hewani). Hivyo hata hela mfanyakazi anayolipwa bado atamailiza kwa matibabu na kusomesha watoto wake.
Kusema kweli nchi masikini hatufaidiki na FDI (foreign investors) kwani free market haiko regulated. Pesa inayochumwa na FDI nchini Tanzania inaishia nchi za nje. Angalia miji mikubwa inayojulikana kama financial capitals of the world (London, New York, Hong Kong & Tokyo) zimejaa banks kubwa ambazo zinaendeshwa shughuli zake kutegemea wawekezaji na pesa toka nchi za nje ikiwemo zinazo flow from Tanzania through FDI. Na pesa hiyo ikiingia Canary Wharf (London financial district - banks) wawekezaji wanapata faida na pesa hiyo inatumiwa na hedge funds for investments, na hao wote (FDI & hedge fund) wanalipa tax toka kwenye pesa hiyo. Hivyo UK government inapata revenue (through tax) ambayo inatumika kununua vitanda hospitals na kutibu wananchi wake bure, kutoa posho pesa kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka 18, huduma kwa wazee, n.k. huku nchi pesa hiyo ilikochumwa ambayo ni Tanzania hao wawekezaji hawalipi tax wala nini, wananchi wa kawaida ni masikini, elimu na huduma ya afya mbaya (viko chini), bali utajiri wote wa nchi na faida wanayopata wawekezaji wageni yaishia mataifa makubwa. Unaona mchezo huo?? Unaona viongozi nchi masikini walivyo walivyo lala? Ndio maana bado tuko masikini ingawa tumekalia utajiri hadi hapo tutapofumbuka macho ndio tutajua tunaibiwa, na siajabu dhahabu, almasi, gas na vinginevyo vitakuwa vimemalizwa
Comment by Mama Malaika on February 18, 2014 at 2:17
Ujue hiyo ya uchumi wa mataifa ya Africa kuweka roho (nchi) rehani kwa wawekezaji tumeshaliongelea sana na mikutano ya viongozi nje. Na mfano mzuri wala si mbali, ni jirani yetu Kaunda (Kenneth Kaunda) wa Zambia kipindi chake cha uongozi kwacha kupolomoka vibaya sana kwa muda wa siku na uchumi kushuka hadi kukatokea state of emergency kupata mkopo wa dharula kidogo nchi iuzwe. Kipindi hicho Zambia ndio ilikuwa inakamata soko la madini ya copper la dunia, na jimbo lote la Copperbelt lilishikiliwa na wawekezaji wageni, na bado lashikiliwa na wageni.
Mwaka jana niliwahi angalia mahojiano kwenye Skynews kuhusu Food Security in Africa, waliongelea kuwa wakati Ethiopia inaomba msaada wa chakula, 90% ya ardhi nzuri nchini Ethiopia iliyoko mto Nile imechukuliwa na wawekezaji toka China, Singapore & South Korea, na chakula chote wanachozalisha kinasafirishwa nchi hizo za wawekezaji na wanauza kwao huku wenyeji wenye ardhi yao wamekumbwa na uhaba wa chakula uliofanya bei ya chakula kuwa kubwa. Raisi asema uchumi umeathirika sana na upungufu wa chakula, hawezi futa mkataba na wawekezaji kwani aliyeiingia mkataba ni raisi aliyefariki.
Comment by Dixon Kaishozi on February 6, 2014 at 8:30

Nitasema nini Mama Malaika ? Nchi ishauzwa hii, Deni la Taifa linazidi kukua wakati tuna rasilimali nyingi ambazo zingetufanya tuepuke kuendelea kukopa na kupata misaada!! Tena Waziri anasimama na kusema deni limekua lakini bado tunaweza kuendelea kukopa!! Matokeo yake sasa ndiyo hali hii ya sasa tunatawaliwa kwa njia ya uwekezaji.. Naamini ni wachache sana tunao elewa hii dhana ya uwekezaji.. wengi wakidhani tunasaidiwa kupata ajira na mambo kama hayo.. ila kwa upande mwingine uchumi wa nchi yetu wote umeshikwa na mataifa mengine kwa jia ya uwekezaji.. Inatia hasira sana!!!

Comment by Mama Malaika on February 5, 2014 at 11:00
Dixon vipi????
Comment by Mama Malaika on February 5, 2014 at 10:59
Wanatukamua kweli kweli @ Tulonge. Kibaya zaidi ni kwamba viongozi wa TZ wanawafata mataifa makubwa na kuwaambia njooni muwekeze na kodi hamtolipa miaka 5. Nyerere hakufanya hivyo.

Yaani kaka yangu Dunda wee acha tu. Nilikuwa nasoma article moja kwenye The Wall Street Journal kuhusu Emerging Markets nilishikwa hasira jinsi Africa ilivyogeuzwa soko la mwenda wazimu.
Comment by Dixon Kaishozi on February 4, 2014 at 8:19

...................................

Comment by Dunda on February 3, 2014 at 22:25

Hahaha hii chungu kwa wenye uwelewa(La Tanzania tuliwafukuza na kuwaita wanyonyaji sasa wanaita wawekezaji)Nyimbo ile ile isipokuwa midundo ya ngoma iko tofauti

Comment by Tulonge on February 1, 2014 at 6:46

Duh! ndomaana hawaishi kuitembelea TZ, cc tunaona sifa na kujisifu tuna urafiki na mataifa makubwa.Ngoja watukamue hadi tubaki mifupa

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*