Tulonge

Maalim Michuzi Jr
 • Male
 • Dar es Salaam
 • Tanzania, United Republic Of
Share

Maalim Michuzi Jr's Friends

 • mohamed selemani kilumba
 • ANGEL NEHEMIAH
 • Oswald
 • BARAKA FRANCO CHIBIRITI
 • Ndekia
 • CataLina Moshi
 • David Ekonjo
 • Lucie
 • Majoy
 • Chui Mfalme
 • mwinyi mpeku
 • mtotomzuri
 • ladymwana
 • Belita
 • Mama Malaika

Maalim Michuzi Jr's Discussions

Wandugu Salamaaaa

Started this discussion. Last reply by CHA the Optimist Sep 25, 2010. 5 Replies

Ni furaha kubwa sana kwangu kuona libeneke la lugha yetu ya kimatumbi inazidi kupamba moto katika mitandao jamii kama hii.shukrani za dhati kwake Dismas kwa kulianzisha libeneke hili la Tulonge kwani…Continue

MTAA KWA MTAA

WASHINDI WA TUZO POINTS VODACOM MKOANI DODOMA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

 Meneja Biashara na Mkakati wa Mauzo wa kampuni ya Vodacom Tanzania, kanda ya kati, Baraka Siwa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya hundi ya shilingi 500,000, mmoja wa washindi wa shindano la Tuzo Pointi, Markfason Haule, mkazi wa Kitinku Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, katika Ofisi za Vodacom Kanda ya Kati zilizopo eneo la Kilimani Jijini Dodoma.
Mshindi wa Shindano la Tuzo Pointi linaloendeshwa na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Ramadhani Mohamedi (kulia) mkazi wa Chang'ombe Jijini Dodoma, akikabidhiwa zawadi ya hundi ya shilingi laki tano (500,000) na Meneja Biashara na Mkakati wa Mauzo wa kampuni ya Vodacom Tanzania, kanda ya kati, Baraka Siwa, makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Vodacom Kanda ya Kati zilizopo eneo la Kilimani Jijini Dodoma.

Klabu Ya Yanga Kupatiwa Uwanja Kigamboni

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) wakati Mkuu wa mkoa huyo alipokuwa akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa viongozi wa Yanga ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.
 Baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati Mkuu wa mkoa huyo alipokuwa akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa viongozi hao ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akipokea baadhi ya nyaraka toka Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwapongeza viongozi wa klabu ya Yanga (hawapo pichani)  kwa hatua waliyofikia katika ununuzi wa uwanja, kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.

Waziri Mwakyembe Azindua Kampeni ya Kuichangia Timu Ya Taifa “Taifa Stars”

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi kampeni maalumu ya kuchangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Maifa ya Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kuanza Juni 21 nchini Misri.
Waziri Mwakyembe amesema watanzania hawana budi kuchangia kiwango chochote na kwamba fedha hiyo itakuwa salama na itawafikia wachezaji hao bila ya mizengwe yoyote.

"Watanzania kote nchini wanaweza kuichangia timu yao  kupitia akaunti zifuatazo BMT N BC 011101000978, Sport Development Fund, CRDB 01J1019956700 na Voda *150*00#5595298. Ukichangia, ujumbe unaopata utume  kwenda 0735 414043 jina litakuja Oscar Zabloni ambye ni mweka hazina ,'' amesema Dkt. Mwakyembe.

Amesema wote watakaochangia watapewa cheti  maalumu na  kiongozi wa kitaifa ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuhakikisha timu yetu ya Taifa inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Naye mwenyekiti wa kamati ya kusaidia Taifa Stars, Paul Makonda amesema siku ya Jumamosi Juni 22, 2019 mkoa wa Dar es Salaam utafanya maombi maalum kwa ajili ya  kuiombea timu ya Taifa Stars ambayo inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili Juni 22 dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal.
Pamoja na mambo mengine Makonda amezitaka kampuni 41 zilizoahidi kuchangia Taifa Stars kutoa michango hiyo.

"Jumamosi ya Juni 22,2019 Mkoa wa Dar es Salaam tutafanya maombi maalum kuiombea timu ya Taifa Stars, na pia nitumie nafasi hii  kuyakumbusha  makampuni  yaliyoahidi kuichangia Taifa Stars sasa wachangie kupitia akaunti hizo,'' amesema Makonda.
Timu ya Taifa Stars iko kundi C, pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya ambapo siku ya Jumapili inatarajia kutupa karata yake ya kwanza dhidi Senegal.

Tayari Stars imeshacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu, huku ikipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Misri 1-0 na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Zimbabwe.
 Katibu wa Kamati ya kuisadia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Mhandisi Hersi Said (kulia)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa harambee maalum ya kuichangia timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paul Makonda.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda akimkaribisha Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Mbunifu wa mavazi akionesha kwa waandishi wa habari vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda (katikati) akijaribu vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji na mashabiki wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto) akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kufuzu kwa timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.
17/06/2019


YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Bungeni jijini Dodoma, Juni 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masala ya Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Bungeni jijini Dodoma, Juni 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 17, 2019. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Latifa Chande. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Pwani, Simiyu watia fora fainali za mita 400 UMISSETA

Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mikoa ya Pwani na Simiyu imeibuka vinara kwenye hatua ya fainali za mbio za mita 400 za mashindano ya  Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha ualimu Mtwara.

Mwanariadha Benedicto Mathias na mwenzake Amos Charles walijinyakulia medali za dhahabu na fedha kwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili kwa upande wa wavulana huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mwanariadha Ismail Tosil kutoka mkoa wa Dar es salaam.

Mwanariadha Benedicto alitumia sekunde 51:30 kumaliza mbio hizo, na Amos alitumia sekunde 51: 50 huku Ismail wa Dar es salaam alitumia sekunde 52:48 kwenye mbio hizo za mita 400.

Kwa upande wa wasichana, medali ya dhahabu ilichukuliwa na mwanariadha Tereza Bernard kutoka Simiyu ambaye alitumia dakika 1:01:22, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Emmy Hosea wa Singida aliyetumia dakika 1:02:35 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rahel Nila kutoka Simiyu aliyetumia dakika 1:03:34.

Katika mchezo wa mbio za kupokezana vijiti wavulana, hatua ya fainali 4 x 400 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Pwani ambao walifanikiwa kujinyakulia medali ya dhahabu baada ya washiriki wake wane kutumia jumla ya dakika 3:39:08 huku nafasi ya pili ikienda mkoa wa Mara ambapo washiriki wake walitumia jumla ya dakika 3:39:22 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa wa Unguja ambapo washiriki wake wane walitumia dakika 3: 40:22.

Katika fainali za mbio za kupokezana  vijiti 4 x 400 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Pwani ambao kwa pamoja wanariadha wake wanne walitumia dakika 4:16:36 na hivyo kuibuka nafasi ya kwanza, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Simiyu ambapo wanariadha wake walitumia jumla ya dakika 4:21:41 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa wa Singida baada ya wanariadha wake wanne kutumia dakika 4: 25:41

Katika hatua ya fainali za mbio za kupokezana vijiti 4 x 100 kwa wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam, nafasi ya pili ilichukuliwa na Unguja na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa Mara.

Mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo kulifanyika mbio za mita 100 kwa walimu,ambapo baadhi ya washiriki walitia fora kwenye mbio hizo kufuatia umahiri mkubwa waliouonyesha wa kukimbia licha ya umri wao mkubwa.

Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kufungwa tarehe 21 juni, 2019 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mtwara.
Mshindi wa kwanza mbio za mita 400 Tereza Benard wa simiyu (mbele) akifuatiwa na mshindi wa pili Emmy Hosea kutoka Singida na nyuma yake ni Rahel Nila kutoka Simiyu mara baada ya kumaliza mbio za mita mia 400 leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
   Mshindi wa kwanza Benedicto Mathias kutoka Pwani, wa pili Amos Charles  na wa tatu Ismail Tosil wa Dar  wakimaliza mbio za mita 400 wavulana asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Baadhi ya wanariadha wa mbio za kupokezana vijiti kutoka mikoa iliyotinga hatua ya fainali wakipokea maelekezo kutoka kwa wasimamizi wa mchezo wa riadha kabla ya kuanza mbio hizo leo asubuhi katika viwanja vya chuo ncha ualimu Mtwara

Gifts Received

Gift

Maalim Michuzi Jr has not received any gifts yet

Give a Gift

 

Maalim Michuzi Jr's Page

Profile Information

Occupation
Baba Lishe
Email Address
othmanmichuzi@gmail.com
Phone No
+255 (0) 713 775 869

Latest Activity

Mama Malaika left a comment for Maalim Michuzi Jr
"Happy Birthday Maalim Michuzi!"
Mar 2, 2014
Mama Malaika left a comment for Maalim Michuzi Jr
"Happy Birthday!"
Mar 2, 2013
Lilian left a comment for Maalim Michuzi Jr
Jul 28, 2011
Joan left a comment for Maalim Michuzi Jr
"Habari yako kaka"
Feb 15, 2011

Maalim Michuzi Jr's Photos

 • Add Photos
 • View All

Comment Wall (23 comments)

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

At 1:12 on March 2, 2014, Mama Malaika said…
Happy Birthday Maalim Michuzi!
At 22:08 on March 2, 2013, Mama Malaika said…

Happy Birthday!

At 21:22 on March 2, 2012, Mama Malaika said…

Happy Birthday!

At 6:49 on July 28, 2011, Lilian said…
At 3:10 on February 15, 2011, Joan said…
Habari yako kaka
At 21:34 on October 28, 2010, Belita said…
MImi nipo kaka Michuzi, hv ww na Issa Michuzi ni diferenti kala one pipo ?hahhaahaha .Ni ndugu yako?
At 14:27 on October 27, 2010, Tulonge said…
Hahhahahahhaaa acha uhuni mkuu, unajifanya umesahau kuwa hujanipa kodi kabisa. Muda wa kukudai umefika acha kuzuga hahahhaaa. Pa1 sana mkuu.
At 21:38 on October 16, 2010, CHA the Optimist said…
PamoJah
At 21:37 on October 16, 2010, CHA the Optimist said…

At 21:57 on October 14, 2010, Moreen said…
Nashangaa huonekani,nikajua wifi amekutaiti sana hadi unashindwa kupumua teh teh teh
 
 
 

© 2019   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*