Tulonge

Tulonge's Blog – June 2013 Archive (98)

Mtoto: Nilipigwa risasi na polisi

“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.

Arusha/Dodoma. Wakati watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na…

Continue

Added by Tulonge on June 18, 2013 at 6:30 — 2 Comments

Mahujaji washauriwa kuahirisha safari za Hijja mwaka huu

JEDDAH-SAUDI ARABIA — Mamlaka nchini Saudi Arabia zimewaomba mahujaji wa ndani na wa nje kughairisha safari zao za HIJJAH za mwaka huu kama kuna uwezekano, kutokana na kazi za ujenzi wa utanuzi unaondelea katika msikiti mtakatifu wa Makkah.Wito huo umetokana kufuatia uamuzi wa serekali kupunguza idadi ya mahujaji wa…
Continue

Added by Tulonge on June 18, 2013 at 1:00 — No Comments

CCM yaishutumu Chadema kuwa ndio wanaohusika na mlipuko Arusha

Wakati jeshi la polisi na vyombo mbalimbali vya usalama vikihaha kumtafuta mtu aliyerusha bomu katika mkutano wa kampeni huko Arusha chama cha mapinduzi CCM kimetoa tamko kuhusiana na tukio hilo na kukishutumu moja kwa moja chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kuwa wao ndio wanaohusika na tukio hilo

Added by Tulonge on June 18, 2013 at 0:42 — 6 Comments

Safari ya Mwisho ya msanii 'Langa'

Hii ni ndiyo nyumba ya milele ya aliyekua msanii wa hip hop 'Langa' ambaye alifariki Alhamisi iliyopita 13/6/2013 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Dar es salaam baada ya kuugua malaria.

Wazazi…

Continue

Added by Tulonge on June 18, 2013 at 0:10 — 2 Comments

Video:Serikali yasema mlipuko uliotokea Soweto Arusha ni bomu la kutupwa kwa mkono


Serikali imesema imesema mlipuko uliotokea katika katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo jijini Arusha na Kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi zaidi ya 70 ni bomu la kutupwa kwa mkono .

Added by Tulonge on June 16, 2013 at 23:49 — 4 Comments

Msimamo wa kundi C baada ya Tanzania kufungwa 4-2 na Ivory Coast leo

Leo watanzania wamevunjwa moyo kwa timu yao kushiriki michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil 2014 baada ya kufungwa 4-2 na Ivory Coast katika mechezo uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar. Matokeo haya yameipa nafasi timu ya Morocco kushika nafasi ya pili katika kundi C baada ya kuifunga Gambia 2-0.

 

Magoli ya mchezo wa leo wa Ivory Coast na Tanzania yalikua kama…

Continue

Added by Tulonge on June 16, 2013 at 23:00 — No Comments

Mbunge Joshua Nassari apigwa katika kituo cha kura Makuyuni Arusha

Nassari akiwa hospitali

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa Na kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani…

Continue

Added by Tulonge on June 16, 2013 at 22:39 — 3 Comments

Baadhi ya Watanzania tuna "F" ya uzalendo

Katika pita pita zangu nilikutana na 'cafe' hii mitaa ya Gongo la Mboto karibu na Kampala University. Ningefurahi sana kama pangeandikwa 'Tulonge Cafe' teh teh teh, au pangeandikwa jina la blog au tovuti yoyote maarufu ya Kitanzania. Hii inaonesha ni jinsi gani watanzania tulivyo kosa uzalendo kwa vilivyo vyetu.

Hata kwenye vyombo vyetu vya habari kama Radio, TV…

Continue

Added by Tulonge on June 16, 2013 at 21:30 — 5 Comments

Polisi watuhumiwa kumuua mahabusu kwa tuhuma ya wizi wa taa ya pikipiki

IGP Mwema

Same. Jeshi la Polisi wilayani Same mkoani Kilimanjaro limeingia katika kashfa nzito baada ya wananchi wa mji huu kuandamana hadi kituo cha polisi kupinga kitendo cha baadhi ya polisi kumpiga mkazi wa wilaya hiyo aliyekuwa mahabusu hadi kufa.

Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa marehemu Maftaha Salimu…

Continue

Added by Tulonge on June 16, 2013 at 6:59 — 3 Comments

Arusha: Kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu chalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto

Kutoka mkoani Arusha Eneo la Soweto ni kwamba mda mfupi kuna mlipuko umetokea katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani uko Arusha kwenye mkutano wa Chama cha demokrasia Chadema katika eneo la Soweto na kuna majeruhi pamoja na vifo vya watu wawili katika tukio hilo...........!!!!

Taarifa za awali toka mlipuko huo kutokea ni kuwa watu waliojeruhiwa katika…

Continue

Added by Tulonge on June 15, 2013 at 20:00 — 3 Comments

Show ya MwanaFA ndani ya Ukumbi wa Makumbusho

Alichokisema Mdau aliyekatiza eneo la tukio:-

Nilikua narudi mjini nikitokea Kigamboni kupumzisha akili. Sasa nikapita pale opposite na iFM kucheki kama Mwana FA kala shavu.

FA katia huruma sana. Yaani mlangoni kulikuwa na wanafunzi wachache wa IFM ambao walikua wakiingia kwa bei ya kandambili.

Jamaa wa mlangoni walikua…

Continue

Added by Tulonge on June 15, 2013 at 8:36 — No Comments

Watu wafurika kwenye 'show' ya Lady JayDee ndani ya Nyumbani Lounge

Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali akiwemo Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu Mbunge wa Jimbo la Mbeya…

Continue

Added by Tulonge on June 15, 2013 at 0:48 — 4 Comments

“Bakora shuleni ni ukatili kwa watoto”

Sophia Simba

Katuma Masamba — SERIKALI imesema inaangalia utaratibu wa kufuta adhabu ya viboko shuleni ili kuweza kufanya mazingira ya shule kuwa ni kimbilio kwa mtoto, badala ya kuwa tishio.

Wakati kauli hiyo ikitolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Zuberi Samataba,…

Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 23:12 — 4 Comments

Serikali yaziruhusu Simba, Yanga kwenda Sudan kuwania kombe la Kagame 2013

Siku moja baada ya Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuziteua timu za URA, Elite Sport ya Chard na Rayon Sports ya Rwanda kuziba nafasi za timu za Tanzania, Serikali jana imetangaza kuziruhusu timu hizo kushiriki michuano hiyo iliyopangwa kuanza Jumanne ijayo Juni 18 Durfur nchini Sudan.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amosi Makalla alisema jana kuwa Serikali ya Sudan imewahakikishia kwa…
Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 22:30 — 1 Comment

Msanii Joh Makini alazwa kwa Malaria kali, ahitaji maombi yenu

Hizi ni tweets za mwanamuziki Joh Makini wa akieleza kuwa ana Malaria kali sana. Awali alienda hospitali akapata matibabu na kurudi nyumbani. Ila hali ikazidi kuwa mbaya ikabidi arudi hospitali kwa mara ya pili ambapo alilazwa.

Taarifa hii ameiweka kwenye twitter.com dk 20  zilizopita toka habari hii iwekwe hapa…

Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 22:30 — 1 Comment

Mmachinga wa Kigamboni akihamasisha watu wanunue sabuni zake vinginevyo atarudia kazi yake ya wizi

Huyu ni mmoja kati ya wamachinga ambao huuza sabuni upande wa Kigamboni karibu na geti la kuingilia/kutokea kwenye kivuko. Kijana huyu huwa ni kivutio kwa watu wanaoshuka kwenye kivuko pale anapokua akinadi bidhaa zake.

 

Zifuatazo ni baadhi ya sentensi zake ambazo hupenda kuzitumia

1) Jamani nunueni sabuni vinginevyo narudia kazi yangu ya…

Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 22:28 — 1 Comment

Kodi ya bia, sigara zazidi kupanda

Dar es Salaam. Serikali imeendelea kuongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi kama ambavyo kodi imekuwa ikifanya kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.

Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara pamoja na waagizaji magari watalazimika kutumia fedha nyingi zaidi ili kupata huduma hizo.

Vilevile baadhi ya bidhaa…

Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 22:06 — 1 Comment

Askari waliofukuzwa kazi watoboa siri

ASKARI 15 wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam waliofukuzwa kazi hivi karibuni kwa kosa la kupokea rushwa ili kupitisha mizigo bandarini kwa njia za magendo wameibuka na kutoa siri ya kufukuzwa kwao.

Mmoja wa askari hao akizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema sababu ya kufukuzwa kwao imetokana na wao kukamata magari ya vigogo serikalini, akiwemo aliyekuwa Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambaye anadaiwa kuwa kinara wa…

Continue

Added by Tulonge on June 14, 2013 at 17:28 — 2 Comments

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*