Tulonge

Tulonge's Blog (2,496)

Vita ya mapato yaibuka Loliondo

Neville Meena na Mussa  Juma, Samunge

MGOGORO mkubwa wa kugombea mapato ya magari yanayokwenda kupeleka wagonjwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila, umeibuka baina ya Serikali ya Kijiji cha Samunge na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.Mgogoro huo ulianza Aprili Mosi, mwaka huu, baada ya halmashauri hiyo kuanza kutekeleza maagizo mbalimbali ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yanayoitaka ikusanye fedha zote zinazotokana na ushuru wa magari.Tangu kuanza kwa utozaji wa…

Continue

Added by Tulonge on April 7, 2011 at 7:08 — 1 Comment

Waliofariki dunia Loliondo wafikia 78

Neville Meena na Mussa Juma, Samunge

IDADI ya watu waliopoteza maisha wakienda kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha imefikia 78.Habari ambazo Mwananchi limezipata na kuthibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi jana zinasema idadi ya vifo hivyo ni ile iliyorekodiwa kuanzia Machi 11, mwaka huu.

"Kati ya Machi 11,…

Continue

Added by Tulonge on April 5, 2011 at 7:00 — 1 Comment

Mjumbe Kamati Kuu awafunda UVCCM

Na Khatib Suleiman, Zanzibar

 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Idd, amewataka UVCCM kuwaepuka viongozi wenye kusababisha mifarakano na kuvuruga malengo ya umoja huo. Balozi Seif, ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alisema hayo jana Nungwi, alipozindua matembezi ya UVCCM kwa ajili ya kumuezi Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume. lisema wapo viongozi ambao hawaitakii mema CCM na UVCCM, na…

Continue

Added by Tulonge on April 4, 2011 at 21:21 — No Comments

Kikwete amlilia Adam Lusekelo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari maarufu, Adam Lusekelo kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku ya Ijumaa Aprili 1, 2011 kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amesema alimfahamu vema Adam Lusekelo kwa jitihada zake kubwa za kuendeleza Taaluma ya Uandishi wa Habari kwa kuandikia magazeti mbalimbali hapa nchini yakiwemo…

Continue

Added by Tulonge on April 4, 2011 at 21:13 — 1 Comment

Rage awataka washabiki wa soka wasihadaike na zawadi toka kwa TP Mazembe

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewataka mashabiki wa soka nchini kutohadaika na fulana pamoja na dola 10 ambazo TP Mazembe wamedai kuwapa watanzania ili wawashangilie, kuchukua zawadi hizo na kuishangilia Simba.Akizungumza jijini juzi, Aden ambaye timu yake inacheza leo, alisema kuwa huu ni wakati wa kuweka pembeni ushabiki na kuzama zaidi kwenye uzalendo ambao ndio silaha kuu katika kila jambo."Unajua…

Continue

Added by Tulonge on April 3, 2011 at 9:48 — No Comments

Maaskofu wengine watinga Loliondo

TIBA ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila imeendelea kushika kasi kufuatia maaskofu watatu wa kanisa hilo kupata kikombe cha mchungaji huyo kisha kushiriki katika kazi ya kugawa dawa kwa watu waliofika kutibiwa.Maaskofu hao waliofika Kijijini Samunge jana asubuhi kabla ya Mchungaji Mwasapila kuanza kutoa tiba, walitetea huduma hiyo wakisema, "Hakuna mwanadamu anayeweza kushindana…

Continue

Added by Tulonge on April 3, 2011 at 9:32 — No Comments

TASNIA ya urembo yakua kwa kasi

TASNIA ya urembo imekuwa ikikua kwa kasi sana nchini kwani wasichana wengi wamekuwa wakijitokeza kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayohusu urembo.

Tunapozungumzia suala la urembo kuna mataji mengi sana yanayoshindaniwa hapa nchini ambapo wengi wetu hufahamu lile la Miss Tanzania.

Tukiachilia mbali shindano la Miss Tanzania pia tunaweza kuweka shindano la Miss Utalii, yaani taji hili hubeba nchini kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuutangaza vyema Utalii uliopo…

Continue

Added by Tulonge on April 2, 2011 at 21:20 — 2 Comments

Kampuni za simu zawachefua wabunge

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jana ilishindwa kupitia taarifa za wadau wa mawasiliano baada wadau hao kushindwa kuwasilisha idadi kamili ya wateja waliosajiliwa katika mitandao yao ya simu iliyopo hapa nchini.

Hatua hiyo ilikuja baada ya watendaji wakuu wa kampuni mbalimbali za simu za mikononi kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya utendaji wa sekta hiyo ya mawasiliano kwa kamati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati…

Continue

Added by Tulonge on April 2, 2011 at 21:12 — No Comments

Magufuli apeleka bilioni 1 Loliondo kwa Babu.

Neville Meena na Mussa Juma, Samunge

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana aliingia katika Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila na kupata kikombe cha dawa, kisha kutangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.

 

Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali itatumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia…

Continue

Added by Tulonge on April 1, 2011 at 2:00 — 2 Comments

"Ung'eng'e" ni kikwazo kikubwa kwa Taifa Stars kufanya vizuri:Poulsen

KOCHA wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jan Poulsen amesema lugha ni kikwazo kinachomfanya ashindwe kufundisha timu hiyo kwa kiwango anachotaka.Akizungumza na Mwananchi, kocha huyo raia wa Denmark alisema pamoja na wachezaji kufanya vizuri bado lugha ni kikwazo kikubwa…

Continue

Added by Tulonge on March 31, 2011 at 23:00 — No Comments

Taifa (TZ) lapata hasara kubwa kutokana na uchakachuaji wa mafuta

*Wafanyabiashara, polisi watajwa

BAADHI ya wafanyabiashara wakubwa na askari polisi ni miongoni mwa wanaotajwa kuhusika kuunda genge la uchakachuaji petroli, dizeli na mafuta ya taa, imeelezwa.Uchakachuaji huo umekuwa ukisababisha taifa kupoteza kati ya sh. bilioni 25 na sh. bilioni 36 kila mwezi.Hayo yalibainika jana mjini Dar es Salaam, kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Fedha na…

Continue

Added by Tulonge on March 31, 2011 at 22:53 — 1 Comment

Makamba: NEC haina uwezo kumng’oa JK

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, amelaani habari iliyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari ‘CCM sasa wajipanga kumng'oa Kikwete’ na kusema ni za uzushi na upotoshaji.Kwa mujibu wa taarifa ya ufafanuzi aliyoitoa Makamba kwa vyombo vya habari jana, habari hiyo ni ya kufikirika."Habari hizi zinapaswa kupuuzwa na viongozi, wana-CCM na wananchi kwa jumla wanaoitakia mema nchi yetu. Habari hizi si za kweli, ni za kufikirika,"…

Continue

Added by Tulonge on March 31, 2011 at 22:47 — 1 Comment

Haya hutokea pale utamu wa kusikiliza hoja unapokolea mjengoni.Unapokuwa umesikiliza hoja nyingi bungeni lazima upate muda wa kutafakari,nadhani huu ulikuwa ni muda muafaka wa kutafakari kwa muheshimiwa huyu.

Added by Tulonge on March 30, 2011 at 7:30 — 4 Comments

Babu Loliondo awasihi wagonjwa kuendelea kutumia dawa za hospitali pia.

MCHUNGAJI Ambilikile Masapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika Kijiji cha Samunge, Loliondo amewataka wagonjwa kuendelea kutumia dawa za hospitali hata baada ya kunywa dawa yake.Akizungumza kijijini hapo jana, Mchungaji Masapila alisema hakuna madhara kwa mgonjwa kuendelea na dawa zake za awali hata baada ya kunywa dawa yake na kwamba si vyema kuacha ghafla kutumia dawa hizo.“Hii dawa yangu inatibu, lakini haizuii kunywa nyingine, unaweza kunywa na ukiona umepona…

Continue

Added by Tulonge on March 30, 2011 at 7:30 — 2 Comments

Jionee maajabu ya Loliondo kwa Babu

Ni mengi sana yamekuwa yakizungumzwa juu ya tiba ya baadhi ya magonjwa sugu ukiwemo ukimwi inayotolea huko Loliondo na mchungaji mstaafu Ambilikile. Jionee yanayotokea huko,pia waweza toa maoni yako.

SEHEMU YA KWANZASEHEMU YA PILI…

Continue

Added by Tulonge on March 27, 2011 at 21:30 — 4 Comments

Majaji 12 wapata kikombe kwa Babu

MAJAJI 12 ambao ni wakuu wa Kanda za Mahakama Kuu ya Tanzania, jana waliingia katika orodha ya vigogo kufika Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.Habari zilizopatikana jana zimeeleza kwamba majaji hao walifika Samunge wakitokea Arusha ambako walikuwa na semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Idara ya Mahakama katika kushughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu.Majaji hao, walifika kijiji hapo majira ya saa saba mchana wakiwa… Continue

Added by Tulonge on November 30, 1999 at 12:00 — No Comments

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*