Tulonge

Uchunguzi wabainisha kuwa Whitney Houston aliuawa

JUU: Whitney Houston enzi za uhai wake akitumbuiza. CHINI: Mwili wa Whitney ukiwa kwenye jeneza ukipakiwa kwenye gari maalumu. KULIA: Mchunguzi wa kujitegemea, Paul Huebl.

Paul Huebl anasema amewapatia FBI ushahidi unaoonesha mwimbaji Whitney Houston mwenye miaka 48 aliuawa kufuatia deni la dawa za kulevya mwezi Februari, mwaka huu.

Mchunguzi wa tiba amethibitisha kwamba Whitney alizamishwa kwenye bafu katika Hoteli ya Beverly Hilton baada ya kutumia mseto wa dawa za kulevya aina ya cocaine, bangi na dawa kadhaa zilizoruhusiwa kisheria.

Jarida la The National Enquirer linaripoti kwamba Huebl anaamini nyota huyo mwenye majanga alikuwa mlengwa wa 'wahusika wenye nguvu katika biashara ya dawa za kulevya ambao waliwatuma wauaji kwenda kudai deni kubwa alilokopa kwa ajili ya dawa hizo.'

Alikuwa akidaiwa na wafanyabiashara hao Dola za Marekani milioni 1.5, kwa mujibu wa baadhi ya ripoti.
Hatahivyo, Huebl alieleza kwamba hafahamu kwa yakini kwamba Whitney alikuwa kauawa - pekee kwamba ushahidi aliopata unaweza kuelekeza katika mwelekeo huo.

Anasema kwamba nyota huyo alipokea mzigo wa cocaine chumbani kwake siku moja kabla ya kifo chake na aliweza kusikika akisema, "Nimechoka na upuuzi huu."

Anasema Whitney hapo kabla alikuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa wauzaji hao waliokuwa wakijaribu kudai deni lao.

Huebl anasema alipata video ya uchunguzi inayoonesha wanaume wawili wasiofahamika ambao walikwenda mara kwa mara kwenye Hoteli ya Beverly Hilton na kujichanganya kwenye msafara wa Whitney.

Mchunguzi huyo wa kujitegemea anadai watu hawa ndio inawezekana waliopenya kwenye chumba cha Whitney hotelini na kumuua.

Pia hakubaliani kabisa na Mkemia Mkuu wa Los Angeles aliyesema kwamba kifo cha nyota huyo kilikuwa ni 'bahati mbaya.'

"Mwili wa Whitney unaonesha wazi majeraha ya kujilinda ambayo yanaweza kuwa yametokea wakati alipokuwa akipambana kuokoa maisha yake," alisema.

Hatahivyo, Huebl alikiri kwamba alama katika mikono yake na kucha cha vidoleni zingeweza kupatikana kwa njia nyingine na kwamba zilikuwa 'zinashukiwa' ni majeraha ya kujilinda.

Mchunguzi huyo wa kujitegemea alisema pia ana ushahidi kwamba chumba cha Whitney hotelini kilikuwa kimepekuliwa, ikionesha viashiria zaidi mapambano ya ugomvi.

Huebl anasema amekabidhi ushahidi wake kwa ofisi ya FBI Chicago kwa matumaini kwamba wakala huyo ataanzisha uchunguzi wa jinai.

"Nafikiri kwamba kama unaweka vitu vyote hivi pamoja, wanaweza kugundua mauaji ya binadamu, kwa herufi kubwa nyekundu "H", alieleza.

FBI hawakuweza kutoa maoni yao kuhusu hili mara moja. Na meseji iliyopelekwa kwa polisi wa Beverly Hills nayo haikuwa na majibu ya haraka.

Huebl, ofisa wa polisi wa zamani Chicago ambaye amegeuka kuwa mwigizaji baada ya kustaafu, anasema amefanya uchunguzi huo baada ya kuwa amekodishwa na mteja mmoja ambaye haamini ripoti rasmi kuhusu kifo cha Whitney.

Anaamini polisi wa Beverly Hills hawakuchunguza kikamilifu kifo cha Whitney sababu hawakutaka kuleta hisia hasi kwa Beverly Hills au kwa Beverly Hilton.

Huebl hakuweza kumtaja ni nani alimkodisha kufanya uchunguzi huo.

Via: ziro99.blogspot.com/

Views: 492

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on December 28, 2012 at 23:47

MH MH MH MAKUBWA TENA HAYA JAMANI HUYU JAMAA ANGERIKUJA NAHUKU TZ KUCHUNGUZA VIFO HATAVYAWATU MASIKINI NIMANI WATAKAMATWA WENGU JUU YA HILI TENA WENGI WAO WAPO KTK SYSTEM

Comment by nestory solile on December 28, 2012 at 16:36

ushauri hasa kwa wanatulonge.kama unataka ufe mapema,uwe kichaa,tukuchangie kam rayc ingawa mama yake anakataa hajachangiwa na mtu isipokuwa jk pekee sijuw hizo hela jk katoa wapi kam si kwa watz mmoja wapo nikiwa mm mlipa kodi,uishie jela basi fuata nyayo za whitney you will perish.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*