Tulonge

Rais Kikwete atangaza matokeo ya sensa 2012.

Rais Kikwete akitangaza matokeo ya sensa 2012

Rais Kikwete ametangaza matokeao ya Sensa ya mwaka 2012 katika Viwanja vya mnazi mmoja jana. Jumla ya watanzania wote ni 44,929,002 ambapo kati ya idadi hiyo Tanzania Bara ni 43,625,434 na Zanzibar ni 1,303,568.

Katika kuhakikisha watanzania wengi wanayapata matokeo haya, ujumbe umekuwa ukitumwa kwenye simu za viganjani za watanzania ikionesha imetoka kwa Rais Kikwete huku ikitaja idadi ya watanzania kwa ujumla na kubainisha idadi ya Bara na Visiwani pia.

Idadi ya watu nchini imeongezeka kutoka watu milioni 34.4 kwa takwimu za Sensa ya mwaka 2002 hadi kufikia watu milioni 44, 929,002 takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ambapo kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwepo na ongezeko la watu zaidi ya milioni 10.

Views: 474

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Monica on January 3, 2013 at 21:44
Mimi nakaa Tegeta Kibaoni hapa bongo,nyumba nne za majiran zangu hawakuhesabiwa,tumetoa
Taarifa serikali za mitaa Hadi ofisi za kata lakini hawakufuatilia..hiyo idadi ni ya kujiridhisha tu
Comment by Mustafa Idd on January 3, 2013 at 21:29

si kweli hiyo si idadi ya watanzania,mi mwenyewe sikuesabiwa sasa je sehemu nyingine haswa huku mashambani?

Comment by Christer on January 3, 2013 at 11:04

TUKO WANGAPI? JIBU LIMEPATIKANA TUKO 44.9 MIL, TULIZANA.

Comment by John Genda on January 1, 2013 at 16:52

ASANTE MHE. DAKTARI  JAKAYA MRISHO  KWA TAARIFA NA HATA MSG ZAKO ULIZOTUTUMIA KWENYE SIMU ZETU TUMEPATA

Comment by David Edson Mayanga on January 1, 2013 at 14:07

HONGERA MH RAIS WETU UNAJITAIDI

Comment by Tulonge on January 1, 2013 at 4:30

kudadeki! Idadi ya Wazanzibar mbona ndogo sana? hata idadi kuwa ujumla itakua pungufu ya idadi halaisi.Ile migomo ya kuhesabiwa ilikua balaa

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*