Tulonge

Morogoro:Jinsi mchezo wa pikipiki ulivyo endeshwa katika hali ya hatari siku ya mwaka mpya

Mshiriki wa mchezo wa pikipiki akiwa hewani huku chini kukiwa na mtoto mdogo.Bahati nzuri mtoto hakuangukiwa na pikipiki hiyo.

NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO.

KATIKA hatua ya kusheherekea sikuu ya mwaka mpya wakati wa mji wa Morogoro jana walishuhudia uhondo wa michezo ya pikipiki uliofanyika ndani ya uwanja wa saba saba huku michezo hiyo ikigubikwa na hatari nyingi.

Moja ya hatari hizo ni pale mshiriki maonyesho hayo Bw Abdul Juma aliponusurika kumuangukia mtoto aliyekuwa jirani na uwanja huo wa saba saba akishuhudia michezo hiyo.

Mbali na tukio hilo pia mshiriki huo nalinusulika kifo baada ya pikipiki, yake kumtupa alipokuwa hewani akionyesha michezo hiyo.

Katika onyesho hilo Mtandao huu haukushuhudia muongozo au ulinzi wowote wa jeshi la polisi,jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hatari hilo.

Akizungumza na Mtandao huu mratibu wa oneysho hilo Bw Athuman Mahita alidai kwamba kila mwaka anaanda onesho hilo mara mbili.

" Hii ni mara ya pili mara ya kwanza nilianda siku ya sikuu ya ldd na mara ya pili ni leo sikuu ya mwaka mpya"alisema Mahita kwa kujiamini.

kwa sasa mchezo huo umevuta hisia za wakazi wengi wa mji wa Morogoro ambao jana walioneka kufulika kwa wingi kushuhudia mchezo huo kwa kulipa kiingilio cha shilingi elfu moja.

Chanzo: dustanshekidele.blogspot.com

Views: 438

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mathias Mlumba Kiyora on January 5, 2013 at 18:24
Tatizo watanzania tumezidi ushamba, kiasi kwamba maafa mengi yanatokea kutokana na uzembe wa baadhi watu.
Ukiangalia hilo tukio la michezo ya pikipiki, watazamaji wamejisahau kiasi kwamba hawajui kama ajari inaweza kutokea.
Hatuna budi sasa tubadilike. Ni hayo tu kwa leo.
Comment by Monica on January 4, 2013 at 9:33
Yakishatokea maafa ndipo serikali inaamka kufuatilia na kupiga marufuku..Hapo si ajabu polisi wanajua na wengine walikuwepo wamevaa kiraia wakiburudisha macho yao.kaaaaaaaaaaazi kwelikweli
Comment by Dixon Kaishozi on January 4, 2013 at 9:07

Mazingira yenyewe na vifaa wanavyotumia ni hatari tupu. vipo ki "local" zaidi!!!

Comment by Christer on January 4, 2013 at 8:49

Mmmmmmmmmmh kweli ni hatari.

Comment by Tulonge on January 4, 2013 at 3:00

Hii ni hatari aisee, huyo mtoto angeweza kukandamizwa hapo chini.Pia naona watazamaji wapo karibu sana na eneo ya kurushia hizo pikipiki. Sina hakika kama walipata kibali cha kufanya michezo hiyo.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*