Tulonge

Hali ya afya ya Msanii Matumaini siyo nzuri

Matumaini

HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji

Kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake

Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa

Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe

"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud

Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini

Matumaini ni msanii kwenye upande wa uchekeshaji.alianza kazi hiyo katika kundi la Kaole na kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie Kiwewe

Chanzo: audifacejackson.blogspot.com

Views: 594

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 3, 2013 at 0:37

Pole yake. Kabla hajaondoka kwenda Msumbiji ilipasa aache akiba ya fedha Tanzania kumsaidia hapo anapopata majanga

Comment by careen mshindo on January 28, 2013 at 8:06
jamaniii...so sad...wamrudishe haraka sana
Comment by Erica Kameka on January 26, 2013 at 20:37

Da pole sana Dada matumaini mungu akujalie upone haraka, tukukusumila fijo kyala agwe na nungwe

Comment by Masha waryoba on January 23, 2013 at 21:45
Duuuh!!Pole sana Dada Matumaini,Tunakuombea kwa Mola,upate afya njema.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*