Tulonge

Iringa: Fundi umeme apoteza maisha juu ya nguzo

Fundi wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mkoani humo. Picha na Geofrey Nyang’oro-Mwanachi

Views: 1982

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by emanuel Lyanga L. on February 25, 2013 at 19:43

HII SI MARA YA KWANZA KWA TANESCO KUUA WAFANYAKAZI, MWAKA JANA 2 ILITOKEA JOGOOO JIJI DAR NAHISI KUNA UZEMBE UNAFANYWA

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 14:12

Poleni wana familia..  Narudisha tuhuma zangu kwa shirika la Tanesco kwa kifo cha huyu fundi!!! Nasema hivyo kwa sababu kuu moja!!! Shirika halijampa huyo fundi TOOLS.. hapo namaanisha VIATU MAALUMU, VAZI RASMI, GLOVES NA VINGINE AMBAVYO KWA NJIA YOYOTE VINGEMSAIDIA ASIPIGWE NA HUO UMEME!!

Angalieni picha vizuri natumaini mtanielewa!!

Comment by Christer on February 25, 2013 at 9:28

Poleni sana familia yake

Comment by ILYA on February 23, 2013 at 14:12

Ni msiba wa watanzania wote ukizingatia alikuwa akitoa huduma kwa jamii ya kitanzania.Lakini nataka kusema nukta hii hapa kwamba:MFUMO WETU WA UMEME TULIONAO KWA SASA TANZANIA SIO SAWA KABISA,UMEKAA KIZAMANI ZAIDI,SIO MFUMO WA KILEO.MIWAYA IMEKAA KAA TU KIAINA ILI MRADI TU IMEKUWE

PI CONNECTION.Kuna haja ya kutizama upya mfumo hu tulionao kwa lengo la kuboresha zaidi na kuwa na mfumo mzuri unaoendana na zama za zeo.

Comment by ABRAHAM PONERA on February 23, 2013 at 13:10

Poleni Familia ya marehemu!

Hao walio washa umeme wachukuliwe hatua kali za kisheria hakuna BAHATI MBAYA, kwani hawakujua kuwa mwenzao anaendelea na kazi? Hapo liko jambo SERIKALI ichukue hatua, lakini utasikia kazi ya Mungu haina makosa na kwamba Mungu alimpenda zaidi, Mungu hapendi kiivyo! Uzembe na Kupenda vinawiana wapi? Wachukuliwe hatua kali.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 23, 2013 at 11:37

Pole fundi ulikua unajenga taifa mungu akuweke mahara pema

Comment by Omary on February 22, 2013 at 22:26

Dah! yaani mimi sitaki kusikia bahati mbaya wakati ushautowa uhai wa mtu yaani watoto wa huyu mchizi watakuwaje?! na shirika kama shirika mtu ukishakufa sidhani kama watasimamia masomo ya watoto wa marehem

me nafikiri hao jamaa au huyo jamaa nae apandishwe pale juu kisha watu wanawasha kama alivyomfanyia mwenzake hivi vifo vya kizembe vitapunguwa maana uzembe wako unatowa uhai wa mwenzako bahatu mbaya haiwezi kurudisha uhai wa mtu bana, na sehemu kama hizo ukiwa na kisa na mtu wanasubiriana mtu anakutowa kafara kisha anasema bahati mbaya yameisha hakuna hiyo nae apandishwe juu ya wire.

Comment by Mama Malaika on February 22, 2013 at 21:54

Jamani... mtu wa watu kaondoka nyumbani asubuhi kwenda kazini ana rudi nyumbani maiti.

MHSRIP!

Comment by eddie on February 22, 2013 at 20:01

Huu ni uzembe. Yaani inasikitisha kuona mtu amepoteza maisha kwa ajili ya uzembe wa wenzake.

Siku hizi naona mashirika mengi ya umeme wamewapa mafundi wao simu za walkie talkie ili wafahamishane nani yuko wapi kabla ya kugusa main switch!!

Comment by Hussein Nkenja on February 22, 2013 at 16:47

Kweli Hellen; Ila nadhani shirika ni lazima lifanye utafiti wa kutosha kushirikiana na jeshi la polisi ili kubaini kama jambo hili lilitendeka kwa makusudi au ni bahati mbaya. Na kama ni bahati mbaya basi shirika linapaswa kuimarisha mawasiliano ya ndani ya kampuni ili kuepusha matukio kama haya. Poleni sana ndugu wafiwa na jamaa wengineo wa karibu na kwa shirika pia.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*