Tulonge

Arusha: Mchungaji aliyedhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na kuchapwa viboko atoa onyo kali

Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.

Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na destruri ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.

Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho.


Chanzo: wavuti.com

Views: 778

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Hussein Nkenja on February 26, 2013 at 10:29

Mchungaji anatakiwa kukumbuka kuwa vita ni vya Mungu na kisasi na juu yake Mungu. Wapo akina Paulo na Sila katika maandiko matakatifu(Biblia) walipigwa na kuvuliwa nguo lakini hakuwa na kisasi, pia mchungaji anatakiwa kufanya hivyo. Ila serikali inatakiwa kufanya maamuzi mazito juu ya wale waliofanya jambo hilo kwa Mtumishi huyu wa Mungu. Watu kama hawa(Wachungaji) huiombea baraka nchi na hivyo kuwadhalilisha si vizuri hata kidogo. Pole sana Mchungaji na Mungu akupe uvumulivu siku zote na uwaombee heri wote waliokuudhi. Asante

Comment by Christer on February 26, 2013 at 9:41

Sure @ Dixon.

Comment by Dixon Kaishozi on February 26, 2013 at 9:08

Pole mchungaji!! Lakini najiuliza uchungaji wake upo wapi ?  Kiasi cha kusema atanunua Bunduki na kuua kama serikali haitachukua hatua!! Mi nadhani hapo kachemka hata kama kadhalilishwa!! Namshauri kutofanya hivyo lasi hivyo atajutia uamuzi wake!!!

Comment by ANGELA JULIUS on February 26, 2013 at 8:00

DUH POLE MCHUNGAJI, HAWA WAFUGAJI WANGEKUWA WANAFANYA HIVI KWA MAFISADI NI UKWELI KABISA UFISADI USINGEKWEPO TANZANIA, KWELI NO HURRY IN AFRICA

Comment by Christer on February 26, 2013 at 7:44

Pole sana Mchungaji tatizo hata ukiripot serikali ya Tz bado haijaamka iko usingizini.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*