Tulonge

Lady Jay Dee: "Wosia wangu kama nikitangulia kufa kabla ya Ruge na Jose Kusaga"

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi

Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.

Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..

Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.

Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.

Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

Chanzo: ladyjaydee.blogspot.com

Views: 1296

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by manka on May 14, 2013 at 15:56

DUH AISEE KUMBE NDIYO HIVI? POLE SANA MY DADA JIDE KWA KWELI HAWAWEZI KUKURUDISHA NYUMA HATA WAFANYE NINI, HATA WASIPOPIGA NYIMBO ZAKO TUTAKUJA KWENYE BAND YAKO, PUMBAVU ZAO  WANAOENDEKEZA  ROHO KUNTU.

Comment by Mama Malaika on May 3, 2013 at 5:58
OMARY... Bongo watu wana nidhamu ya woga na ndio sababu uonevu hautokwisha. Watu wenye rangi na wenye pesa wanatukuzwa na kusujudiwa kama miungu na kuogopwa. Jifanye hivyo UK watakuanika Live hawaangalii wewe ni Iron Lady (Margaret Thatcher) au mtoto wa Malkia Elizabeth.
Mie tu mzazi nikikosea wanangu wanijua juu na kunichana Live, baba yao anambia ni apologize kwa watoto. Inabidi tu niwe mpole na kuomba yaishe. Watoto wa kizungu balaa, na hiyo imefanya wenzetu kutokuwa na nidhamu ya woga na pia kuwa more independent toka utotoni.
Comment by Omary on May 2, 2013 at 19:46

Unajuwa sikuhizi ile nidhamu ya uoga inatakiwa ituondoke mtu akikukosea na ukiwa na uhakika unamchana live bila chenga atajiju hahahah maana tukiogopa tutazidi kuonewa maisha yote mtu kakukanyaga unavumilia kwakuwa ana pesa hakuna hiyo kama ana pesa ni zake na watoto wake wewe hazikusaidii kitu unatafuta vyako kivyoko kwanini akuifuate?! hao sisi tunaita kupe kama yasemwayo yana ukweli hakuna haja ya kumficha mtu mwambie ili aache tabia hiyo aridhike na alichonacho.

Comment by Omary on May 2, 2013 at 19:38

Daffa nilikutumia Kaka.

Yes nina Office kule kaka najaribu jaribu si unajuwa maisha magumu.

skype id yangu ni: faisal.omary

Comment by MGAO SIAMINI,P on May 2, 2013 at 14:34

kumbe sio siasa tu hata mziki,mibaba mizima hovyoooooo! kupimana nguvu na wanawake kwetu sie mwiko. mnazuia maendeleo ya muziki Tanzania

Comment by OBED KITALIKA on May 2, 2013 at 13:44

Pole sana Lady Jay Dee, kumbe ule wimbo wa "......nasonga mbele mangapi nimeona.... Hamchoki..." Kumbe uliwalenga hao hao watani zako???

Jay Dee kwa kuwa ni watani zako huenda wanakutania.

Comment by Mama Malaika on May 2, 2013 at 9:57
Kaza buti Jide, yakikushinda bongo tafuta sehemu nyingine kwani wana muziki sasa wanafanya shughuli zao nchi yeyote ile.
Comment by Mama Malaika on May 2, 2013 at 9:45
Khaaaa.... Joseph (Kusaga) noma miaka yote hiyo haridhiki? Tabia hii ya ufisi ku-control wanamuziki kaianzia mbali hata kabla Clouds haijaanzishwa. Alikuwa middle man wa small bands zinazotaka tumbuiza Hotels za beach enzi zile Silver Sands & Bahari beach hotels zavuma sana na pia kwa marehemu Mzee Mwakitwange (Rungwe Oceanic) kunaisha ishia. Kioindi hicho Joseph alikuwa bado mdogo ki umri ila alikuwa anawakamua si mchezo, tena bands nyingine ni za watu umri wa babu yake enzi hizo. Tamaa kuendekza pesa ni mbaya sana INAPOTEZA UTU.
Comment by patrick naiman on May 2, 2013 at 9:00

SAAFI JAY DEE,MAKAVUUU LAIVUUU!

Comment by Mjata Daffa on May 2, 2013 at 8:46

Omy usimpe kichwa huyu dada, mm nadhani kupambana na mwenye pesa nisawa nakucheza na kaa la moto, dada yetu kajiamini sana sasa kwakutaja majina ambayo mm binafsi naogopa hata kuyarudia. nadhani alikosa mshauri mzuri any way mdomo ni mali yake nakatiba inampa uhuru wakuongea.

SASA OMARY Mbona unanibania SKYPE ID yako? nimekuomba juzi kimya halafu jana nilipita kwa wakala wa TIGO Pesa G/MBOTO kuungeza salio langu nikaona jina lako linatumika kama wakala unaofisi kule? 

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*