Tulonge

“Bakora shuleni ni ukatili kwa watoto”

Sophia Simba

Katuma Masamba — SERIKALI imesema inaangalia utaratibu wa kufuta adhabu ya viboko shuleni ili kuweza kufanya mazingira ya shule kuwa ni kimbilio kwa mtoto, badala ya kuwa tishio.

Wakati kauli hiyo ikitolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Zuberi Samataba, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba ametaka watoto wanaozaliwa magerezani wasifanywe kama wafungwa, bali wapatiwe haki zao za kimsingi ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu.

Simba alisema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza katika mkutano wa kujadili utafiti uliofanywa juu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Alisema suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto bado ni tatizo na utafiti huo umeonesha ukatili unafanyika shuleni, nyumbani na maeneo mengine, unadhoofisha ukuaji wao wa kimwili na kiakili, bila kujali kama unafanywa na mwanafamilia au mtu mwingine ni ukiukwaji wa haki na misingi ya watoto.

“Hapa tumekutana kujadili ni wapi tumefikia katika harakati za kupinga ukatili wa jinsia kwa watoto na akinamama kwa ujumla lakini bado upo japo kwa kiasi kikubwa tumeweza kupambana nao. Hata bakora shuleni bado ni ukatili kwa watoto kwa sababu zinawafanya waone shule ni mazingira hatarishi kwao, jamii lazima ibadilike na kuona umuhimu wa mtoto,” alisema Simba.

Chanzo: HabariLeo

Views: 567

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on June 18, 2013 at 9:57

Kweli kbs, viboko sio suluhu la mtoto kuelewa/kuwa na tabia nzuri. misingi ya mtoto ikijengwa vzr na wazazi hata shulen hatuhitaji viboko.

Comment by Silas A. Ntiyamila on June 16, 2013 at 14:55

Jamni kizazi gani tunatengeneza? maana wenetu hawachapi vboko kwa sababu ya mazingira sasa huku kwetu watoto 100 darasani mwl atawawza bila viboko?

Comment by ANANGISYE KEFA on June 15, 2013 at 10:06

ishu siyo viboko ila ni mitaala mibovu wewe mtoto wa darasa la kwanza ile kunusa shule tu anaanza na masomo karibu nane halafu na viboko juu unadhani hapo atapenda shule kweli. mimi nakumbuka kipindi kile naanza shule darasa la kwanza na la pili tulikuwa tunasoma masomo matatu tu nayo ni kusoma kuandika na kuhesabu halafu ni full kuimba na kucheza hapo unamjengea mtoto mazingira ya kuipenda shule mnapofika darasa la tatu hapo ndipo shule rasmi inapoanza na masomo yanaongezeka mpaka saba.

Comment by Tulonge on June 14, 2013 at 23:13

Mmh! kuna mitoto imepinda balaa.Bila mboko aiendi kabisa.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*