Tulonge

Kenya: Aliye vuliwa nguo na polisi ili kubaini jinsia kulipwa

Mwanamume aliyevuliwa nguo na polisi ili wathibitishe jinsia yake, atalipwa ridhaa ya Sh200, 000 na Serikali kwa kuvunjiwa heshima. Mwanamume huyo ana tatizo la kujitambua kijinsia (Gender Identity Disorder) na huvalia nguo za kike.

 

aji Mumbi Ngugi alisema maafisa wa polisi katika kituo cha Thika walikiuka haki za Alexander Ngungu Nthungi kwa kumvua nguo adharani.

Jaji Ngugi aliamuru Serikali imlipe ridhaa hiyo ya Sh200,000  Bw Nthungi anayetamani kuvaa nguo za kike.

Jaji huyo alisema polisi hawakuwa na ruhusa au idhini kisheria kumvua nguo mlalamishi na kwamba “kile wangelifanya ni kumpeleka hospitali apimwe jinsia yake na daktari.”

“Kwa kumvua nguo hadharani umma ukitazama na waandishi habari, polisi walikuwa na lengo la kumwaibisha kwa vile alikuwa amevalia kama mwanamke. Ni jambo la kusikitisha hata kwamba vyombo vya habari vilichangia katika kumvunjia heshima na siri yake kwa kutangaza hali yake,”akasema Jaji Ngugi.

Nthungi aliiambia mahakama katika ushahidi wake kwamba ijapokuwa alizaliwa akiwa mwanaume anafurahia kuvalia nguo za kike.

Siku hiyo ya Januari 14,2011 mlalamishi anasema alikuwa katika kibanda chake cha kuuza mboga na alikuwa amevaa kama mwanamke. Polisi walimkamata na kumpeleka katika kituo cha Makongeni kumhoji kufuatia madai alikuwa amempiga na kumuumiza mwanamke mwingine.

Walipofika katika kituo cha polisi, maafisa wa usalama waliwaita wananchi na waandishi habari katika kituo hicho kushuhudia ikithibitishwa ikiwa alikuwa mwanamke au mwanaume.

Kumpapasa

“Ni wakati huo afisa wa polisi mwanamke aliponivua nguo mbele ya umma na waandishi habari ithibitishwe ikiwa mimi ni mwanaume au mwanamke,” Bw Nthungi alisema.

Alidai alisononeka afisa huyo alipompapasa na hata kumfuta nywele, kumpiga na kwamba kitendo hicho kilimvunjia heshima na kumsababisha aone aya na aibu. Hatimaye alienda kupata mashauri katika hospitali kuu ya daraja la 5 la Thika.

Jaji Ngugi alisema ni kinyume cha sheria kumvua mtu adharani mbele ya waandishi habari hata ikiwa mmoja ni mwanamke au mwanaume.

Jaji huyo alisema hakuna  makosa kwa afisa wa polisi mwanamke kumkagua mahabusu mwanaume.

Views: 741

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on June 19, 2013 at 16:59

MAKUBWA

Comment by MGAO SIAMINI,P on June 19, 2013 at 13:21

kweli huu uhuru unatuletea maajabu haya twendelee tuone

Comment by Samwel Mnubi Masatu on June 19, 2013 at 2:02

hayo makubwa

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*