Kushoto ni Admin wa tulonge.com(Dismas) akikabidhiwa zawadi zake na Kala Jeremiah
Mnamo tarehe 28 Juni 2013 msanii bora wa Muziki wa HipHop Tanzania Kala Jeremiah alitangaza shindano kupitia ukurasa wake wa Facebook. Alitaka wadau waupige picha ukurasa wake wa facebook siku ambayo utafikisha 'likes' 44,444. Mdau wa kwanza kupiga picha hiyo na kutumtumia kwenye 'inbox' yake ndiye mshindi.
Bahati nzuri Admin wa tulonge.com (Dismas Hiza) ndiye aliyebahatika kuwa wa kwanza kutuma picha hiyo na kujishindia sh. 100,000 pamoja na 'Audio Album' ya msanii huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Mlimani City, DSM.
Stori zikiendelea baada ya kutia changu mfukoni teh teh teh
Picha ya ukurasa huo ilionekana hivi:-
Add a Comment
hahahhahaahaaa hapana mkuu Swedi, wala sikua naivizia. Ilitokea tu siku hiyo nafungua page yake nikazikuta zipo hivyo. Ndo nikakumbuka kuwa aliwahi kutangaza shindano hilo
Mzee Unaonekana ulikua unaivizia kinoma kinoma hyo namba. au uliweka ka software uka ka configure ikifika tu kapige alarm Hahahahahah... Hongera sana mzee dis.
Teh teh teh niliiotea balaa hadi watu wakashangaa. Nadhani kilichonisaidia ni kuweza kuituma HARAKA kwenye inbox ya Kala kabla ya wengine.According to Kala watu zaidi ya 200 waliiona page ikiwa na hizo likes 44,444 na walimtumia, ila mimi nilikua wa kwanza kumtumia @Silas
Mwana wewe noma, uliibahatishaje? unabahati kama yangu kipindi kie cha pamja
Asanteni Magao & Mama
hongera
Hahahaaaa Chaoga hela iliishia hapo hapo Mlimani City.Baada ya kukabidhiwa tu nikazama Shoprite, nilipotoka humo ndani nakumbuka nilikua na hela ya nauli tu ya kunifikisha kwangu teh teh teh
DAAH SAFI SANA AISEEE NA MIE NGOJA NIWE WA KWANZA KUKOMENTI HAPA NAWEZA DONDOSHEWA CHENJI YA KIROBA,
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge