Tulonge

Hatimaye Msanii Lulu arudi darasani rasmi

Msanii Elizabeth Michael a.k.a Lulu

Hivi karibuni Msanii wa Filamu za Kitanzania Elizabeth Michael (Lulu) alitangaza nia yake ya kurudi darasani ili kujiendeleza kielimu. Lulu ametimiza ahadi yake baada ya kujiunga na Chuo cha Magogoni (Tanzania Public Service College). Tulonge.com ilifanikiwa kuongea na Mwalimu wa Lulu ambaye hakupenda jina lake litajwe na kuthibitisha kuwa ni kweli ameanza kusoma kozi ya 'Certificate in Records Management' .

 

Kwa sasa ameanza kusoma hatua ya awali (Foundation Course) kabla ya kuanza masomo kamili ya ngazi ya cheti cha 'Records Management'. Sababu ya kuanza na 'Foundation Course' ni kukosa vigezo vya kujiunga moja kwa moja na ngazi ya cheti ya kozi hiyo.

 

Hadi sasa ana muda wa usiozidi wiki moja chuoni hapo. Mwalimu wake aliieleza tulonge.com kuwa Lulu ameonesha kujiamini sana awapo darasani kwa kujibu maswali na kuchangia mada tofauti pale anapohitajika kufanya hivyo.

 

"Lulu anaonekana ana kichwa kizuri, japo hana muda mrefu darasani lakini anaonesha kujiamini sana katika kujibu maswali na kuchangia mambo mbalimbali". Alisema mwalimu huyo.

 

Kama ilivyo kwa mastaa wengine, pia Lulu amekua akitolewa macho sana na wanachuo wenzake awapo darasani au nje.

 

Tulonge inamtakia mema katika masomo yake.

Views: 1385

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Swedi on August 26, 2013 at 10:22

Tumuombee mungu asome na atulie maana ukishazoea night club kurudi nyuma ni kazi ya ziada.. zile night club katika imani yangu tunaita ni chuo cha shetani au ibilisi sasa ukishaingia huko hakuachii kirahisi. So tumuombee huyu binti asirudi tena kule na akomae na shule yake na afanye yake ya msingi ya kumuinua kimaisha

Comment by Christer on August 15, 2013 at 10:08

Good.

Comment by hamsey haroun on August 7, 2013 at 10:34

hongera kwa uyu mtoto muhimu akazane kusoma

Comment by ANANGISYE KEFA on August 7, 2013 at 7:35

kweli alikuwa chuo cha mafunzo

Comment by Mama Malaika on August 6, 2013 at 23:38
Bora kaamua kusoma. Namtakia masomo mema, natumai sasa ametulia na foolish age imepita

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*