Tulonge

Serikali inacheza ‘makida makida’ suala la Dk Ulimboka

Umepita zaidi ya mwaka mmoja tangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mengi yalisemwa kutaka kujua chanzo cha utekaji huo, hasa ikizingatiwa kuwa Dk Ulimboka aliongoza mapambano ya madaktari dhidi ya Serikali wakidai masilahi zaidi. Hata hivyo gazeti la MwanaHalisi ambalo sasa limefungiwa, katika toleo lake moja liliwahi kuchapisha habari ya uchunguzi huku likimtaja moja wa watu wanaodhaniwa kuwa maofisa ya Idara ya Usalama wa Taifa kuhusika na tukio hilo.

Madai hayo yalikanushwa vikali na idara hiyo na kilichofuatia baada ya hapo ni kufungiwa kwa gazeti hilo.

Badala yake Jeshi la Polisi lilimtia mbaroni raia wa Kenya, Joshua Gitu Mhindi (32), aliyedai kushiriki kwa utekaji na utesaji huo.

Julai 13, mwaka jana, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ilimkamata Muhindi na kumfikisha

mahakamani na kusomewa mashtaka ya utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk Ulimboka.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alifafanua kuwa mtu huyo alifika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kawe, jijini Dar es Salaam akitaka kuonana na Mchungaji Joseph Gwajima bila mafanikio na ndipo alipokutana na Mchungaji Joseph Kiriba na kumweleza kuwa yeye ni mwanachama wa kikundi cha Mafia ambacho hukodiwa kufanya matukio ya kihalifu nchini Kenya na nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Baada ya kesi hiyo kutua Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa zaidi ya mwaka mzima, majuzi Mahakama hiyo imemwachia huru kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea kumshtaki.

Baada ya kuachiliwa, eti jeshi hilo likamkamata upya na kumfungulia kesi nyingine ya kulidanganya jeshi!

Ama kweli haya ni maigizo, hivi kwa akili ya kawaida tu, mtu wa genge la mafia anaweza kujisalimisha polisi na polisi wakaridhika tu bila kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kumpeleka mahakamani?

Kichekesho kingine ni kauli ya DPP, Eliezer Feleshi kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kuwakamata waliomteka Dk Ulimboka na kuwa kiongozi huyo wa madaktari hatoi ushirikiano. Kauli hiyo ya Feleshi imekuja wakati tayari Dk Ulimboka kupitia wakili wake Nyaronyo Kicheere alishatoa andiko lake la kiapo huku akimtaja mtu yuleyule aliyetajwa kwenye gazeti la MwanaHalisi kuhusika na utekaji huo.

Sijui Feleshi na Polisi wanataka ushahidi gani au kwa nini wameweka pembeni ushahidi huo na kumng’ang’ania Mkenya huyo? Nionavyo polisi wanacheza makida makida katika suala hili.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 430

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Swedi on August 21, 2013 at 12:28

TZ Nchi yetu kuna watu wanaostahili kuishi na wengine ni basi tu tupo kujaza idadi hata ukiuliwa hapo wala hakuna anayestuka. Wamejipachika madaraka ya Mungu!!! Anaweza akakuua alafu Haulizwi anaonekana hana Hatia sasa sijui wewe unayeuliwa ndio mwenye Hatia.. Hebu angalia Marehemu MWANGOSI pale Nyololo Iringa... Aaaaah!! Shiit

Comment by Dixon Kaishozi on August 14, 2013 at 17:24
Dada angu.. usitapike bure. HAO ALIO WATAJA WAMECHUKUKIWA HATUA GANI ? KAMA ALIOWATAJA WAMEPOTEZEWA.. ATAKAO WATAJA TENA NDIYO WATACHUKULUWA HATUA ? kamtazamo kangu tu.. tehee
Comment by ANGELA JULIUS on August 14, 2013 at 17:02

NIPENI LIMAO NASIKIA KUTAPIKA, MUHUSIKA AMESHASHIBA PESA AMEKAA KIMYA OH NITAWATAJA OH NITAFANYA VILE CHEZEA PESA WEWE UTALOWAAA

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*