Tulonge

Polisi nchini Uchina imetangaza kuwa itatoa zawadi kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kumkamata mama mmoja ambaye anashukiwa kumng'oa macho mvulana mwenye umri wa miaka sita.

Shambulio hilo linasemekana kutokea tarehe ishirini na nne mwezi huu katika eneo na Fenxi, iliyoko katika mkoa wa Shanxi.

Mvulana huyo anasemekana alikwenda kucheza na watoto wengine lakini wazazi wake walimpata baadaye huku macho yake yote yakiwa yamengolewa huku akivuja damu.

Mvulana huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu hospitalini.

Idara ya polisi nchini humo imetoa zawadi ya zaidi ya dola elfu kumi na sita kwa yeyote atakayetoa habari, kuhusu aliyehusika na shambulio hilo.

Wazazi wa mtoto huyo wanasemekana kuwa wakulima.

Mamake amesema mtoto huyo aliwaambia kuwa wakati alipokuwa akitembea alishambuliwa na mama mmoja ambaye hakumfahamu.

Polisi walipata macho ya mvulana huyo karibu na eneo la tuko.

Uchunguz wa awali umebainisha kuwa sehemu ya mboni au Cornea kwa Kiingereza ilikuwa imengolewa, na hivyo kuashiria ulanguzi wa viungo vya kinadamu.

Hata hivyo polisi wanasema hawajatambua chanzo cha shambulio hilo.

 

BBC Swahili

Views: 592

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on September 2, 2013 at 11:31

Pole dogo.. Hiyo pesa wangepewa hao wazazi wake iwasaidie katika malezi ya huyo mtoto!!!

Comment by Swedi on August 30, 2013 at 10:53

Ochu hujui kama kuna watu wanampa pole wengine wanamuahidi kumsaidia msaada wa matibabu kupitia hiyo hiyo galax angefanyaje sasa kaka

Comment by KUNAMBI Jr on August 30, 2013 at 10:42

mtoto hana macho maza ndo kwanza anaangalia Galaxy yake duuh

Comment by jemadari mimi on August 30, 2013 at 9:57

pole sana dogo

Comment by manka on August 29, 2013 at 17:29
ee Mungu mpe huyo mwanamke shetani adhabu inayomstahili
Comment by Tulonge on August 29, 2013 at 12:31

Fikiria unarudi nyumbani unakuta mwanao katolewa macho.Hata sielewi nini kitatokea

Comment by Swedi on August 29, 2013 at 11:57

Pole Mama Malaika Ujue Jicho Ndio linalohusika na ndio lililotendwa sasa lazima machozi yakutoke,, Duuh hv mtu ukiwa katika harakati za kutekeleza hilo zoezi unakua umekula mabangi au unakua na akili zako timamu!! too sad too bad

Comment by Agnes Nyakunga on August 29, 2013 at 10:05

ee mungu hebu ona viumbe vyako hawana hata roho ya huruma kwa kweli huyo mwanamke alaaniwe!

Comment by Mama Malaika on August 28, 2013 at 23:40
Machozi yamenitoka nilivyoona habari hii kwenye Skynews. Biashara ya viungo vya binadamu imeshamiri sana Asia.
Comment by Tulonge on August 28, 2013 at 23:36

Daah! inasikitisha sana

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*