Tulonge

Mbeya: Baba wa wale watoto waliotelekezwa akamatwa

Watoto Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakifanya usafi katika nyumba wanayoishi leo.

JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda kata ya Iyela Jijini Mbeya akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi mitano bila huduma za msingi ikiwemo chakula na sare za shule.

 

Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka huu eneo la nyumbani kwake alikokuwa amewatelekeza watoto hao.

 

Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria dhidi yake baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili kesi iliyombele yake.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa uchunguzi unafanyika ili kesi iweze kufunguliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vikomeshwe.

 

Wakati huo huo maisha wanayoishi kwa sasa watoto hao Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila huduma za msingi wasamaria wema wameombwa msaada wao wa hali na mali.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada kutoka kwa walimu na baadhi ya watu ambao huwapa unga na maharage na wao hulazimika kutafuta fedha za kununulia mahitaji mengine kama mafuta ya kula na taa.

 

Wametaja baadhi ya mahitaji yao muhimu kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule kutokana na kuchakaa kwa sare wanazotumia ikiwemo Madaftari, kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, sabuni, chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage.

 

Aidha imeshauriwa kuwa kutokana na mazingira wanayoishi watoto hao kutokuwa mazuri kwa utunzaji wa vyakula ambapo nyumba wanayoishi kutokuwa na mlango vitu hivyo vihifadhiwe Ofisini Kwa Mwalim Mkuu kama vitapatikana.

 

Kwa yeyote atakayekuwa ameguswa na hali ya watoto hao awasiliane na Mbeya yetu kupitia namba 0754374408 au Bomba fm redio kupitia 0754 490752.

Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwa na watoto hao alipowatembelea nyumbani mara baada ya kuwakosa shuleni mwandishi wetu alipowauliza kwanini hamjaenda shule leo? wakamjibu tulijua leo ni sikukuu ndiyo maana hatujaenda shule

Wakiwa na waalimu wao

Na Mbeya yetu Blog

Views: 1159

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on October 17, 2013 at 17:08

dah inasikitisha sana sina la kusema nwaombea kila la kheri asante kwa number za simu Tulonge

Comment by Tulonge on October 16, 2013 at 21:41

Abraham Ponera mwambie Hamis ajiunge tulonge, tunahitaji mchango wake.

Comment by ABRAHAM PONERA on October 16, 2013 at 20:38

comment by Hamisi S. Nyema, ADEM,Bagamoyo. Inashangaza kuona watoto wakipewa mateso na wazazi wao waliokunaliana kuwazaa, wapimwe akili zao iwapo ziko sawasawa. Sheria ichukue mkondo wake  lakini adhabu izingatie kuwa makuzi ya mtoto huwa bora zaidi wanapolelewa kwa mapenzi ya wazazi. Kwa kipindi hiki cha mpito watoto hao walelewe kwenye kituo bora na wapewe mahitaji maalum ukiwemo ushauri na michezo mingi itakayowasahaulisha mateso waliyoyapata ili kuwarejesha katika hali ya kawida.

Comment by ABRAHAM PONERA on October 16, 2013 at 20:14

Itapendeza kuona kweli mzazi huyo anafikishwa kwenye vyombo vya sheria na itasikitisha kuona mnyanyasaji huyu akiachiwa huru bila kuchukuliwa hatua zozote, hata hivyo jeshi la polisi lina mkono mrefu litumie njia zote ili kumsaka mzazi wa kike wa hao watoto, pia wakati huu serikali iwatunze watoto hao na si kuwaachia wasamaria wema.

Comment by Chikira Chikira on October 16, 2013 at 12:30

Inasikitisha sana kuona wazazi wanatelekeza watoto wao kwa muda wote huo!! hata kama mtu unashida kiasi gani huwezi kukimbia familia na kuacha watoto wadogo kiasi hiki ambao hawajajitegemea!! too bad  for the litle kids to have such unspeakable parents!!!

Lakini tuwaombe hao waalimu wa shule wanakosoma hao Malaika wa Mungu, wawachukue nyumbani kwao, si kuwatunzia tu chakula na kuwapa wanapo kihitaji! hao watoto bado ni wadogo sana kuishi maisha ya kujitegemea jamani!! vyombo husika navyo vichukue hatua stahiki kwa wazazi hao ili kukomesha unyama huo!!!  Tunashukuru kwa namba za simu, tutaweza kutoa michango yetu kadiri Mungu atavyotujalia!!!

 

Comment by David Edson Mayanga on October 16, 2013 at 12:24

INATIA SIMAZNIKUBWA SANA JUU YA HAWA WATOTO UNAWEZA HATA TOACHOZI UKUWAUNAPATA HABARI KAMA HII ILA IPOSIKU NAWAFIKIA WATOTO KAMA HAWA NAKUTATUA MATATIZO KATIKA JAMII KWASASA NAWATIAMOYO WALE WOTE WALIOWEZA FIKA KTK ENEO LA TUKIO NAKUTOA MSAADA KWA WATOTO HAO

Comment by Mama Malaika on October 16, 2013 at 8:10
Kwa jinsi hawa watoto wanavyopata shida, huyo baba na mama yao Mungu Kesha walaani. Haiwezekani mzazi ukatenekeza watoto wako kihivi, la sivyo una laana. Hata vichaa waishio barabarani hawafanyi hivyo
Comment by Mama Malaika on October 16, 2013 at 8:02
Asante sana Dismas kutuwekea hizo tel numbers. Mungu akubariki

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*