Tulonge

Ndugu wa Mushi, mchumba wa Ufoo watilia shaka madai kuwa marehemu alijiua

Imeandikwa na JESSICA KILEO, Gazeti la Uhuru — FAMILIA ya aliyekuwa mzazi mwenzake, Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, Anthery Mushi (40), imevunja ukimya na kudai inapata wakati mgumu kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe. Imesema suala hilo inaliachia Jeshi la Polisi lishughulikie ili kubaini undani wake.

Kaka wa marehemu, Isaya Mushi alidai hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wawakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa.

Mushi alidai wapo katika wakati mgumu wa kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe, kwani haiwezekani mtu akajipiga risasi sehemu mbili ambazo ni kidevuni na upande wa bega la kushoto.

Alidai sio kazi yao kutoa hukumu, kwani wanasubiri upelelezi wa polisi kutoa jibu lililo sahihi kuhusiana na tukio hilo.

Baada ya kifo cha ndugu yetu, wanafamilia tulifanya uchunguzi wa awali na bado linatuwia vigumu kutambua upi ni ukweli kuhusu jambo hilo kuhusiana na kifo hiki,' alidai.

Kaka huyo alidai katika uchunguzi wa madaktari, walibaini kuwa marehemu alijipiga risasi mbili sehemu tofauti.

Akisoma risala kwa waombelezaji, Mushi alidai marehemu alizaliwa Januari 3, 1973 katika kijiji Uru Ongoma Timbirini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. Alisoma Shule ya Msingi Ongoma Timbirini kutoka mwaka 1981 hadi 1987 na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Zanzibar na baadaye alisoma kozi mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari. Mwaka 1994 alijunga na Kituo cha Televisheni cha ITV na mwaka 2002 alikwenda STR na hadi mauti inamkuta alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa, Sudan, akiwa mtaalamu wa habari.

Dada wa marehemu, Eviolatha Mushi alisema alipokea kwa masikitiko msiba wa mdogo wake kwa sababu alikuwa mtu mwelewa na msikivu katika jamii ambayo wamekulia. Eviolatha alitoa wito kwa wanandoa kumshirikisha Mungu katika maisha yao na sio mwanadamu, hali itakayosaidia kutatua matatizo wanayopitia kwa kuwa neno la Mungu linasema kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke lazima atalamba mauti, hivyo hawana budi kukubaliana na neno hilo.

Mdogo wa marehemu, Happy Mushi, alisema hadi sasa hawezi kuamini chochote hadi polisi itakapotoa majibu ya upelelezi. Alisema Oktoba 9, mwaka huu, marehemu alimpigia simu na kumwambia anamshukuru Mungu, kwani ametoka kufanya kazi katika mazingira magumu, hivyo muda si mrefu anaweza kuhamia Tanzania, na kwamba yupo nchini kwa ajili ya kumalizia nyumba yake ambaye ipo Mbezi, Dar es Salaam.

Lakini cha kushangaza kabla ya wiki alisikia katika vyombo vya habari vikitangaza kaka yake amejiua mwenyewe pamoja na familia ya mke wake,' alisema.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda kijijini kwao Ongoma Timbirini na unatarajiwa kuzikwa leo.

Wakati huo huo, Ufoo aliyelazwa Muhimbili hali yake imetengemaa na ameanza kutembea pamoja na kwamba daktari anayemhudumia anakataza watu kuingia kumtazama.

Ofisa wa Habari wa MNH, Aminiel Eliegaisha, alisema jana kuwa, Ufoo anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya kutembea, ingawa bado hawajaanza kuwaruhusu watu kwenda kumtaza kwa sababu ameshonwa sehemu nyingi na kwamba wanahofia kidonda kutokupona haraka.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Oktoba 13, mwaka huu, eneo la Kimbamba nyumbani kwa wazazi wa Ufoo, ambapo alikwenda akiwa na mzazi mwenzake Anthery Mushi. Iliripotiwa kuwa Mushi alimuua mama wa Ufoo kwa kumpiga risasi zinazosadikika tano na kumjeruhi kabla ya kujiua mwenyewe.

via: wavuti.com

Views: 973

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on October 21, 2013 at 16:18

ni mtoto mwenye akili zake ambaye unaweza kumtuma a barabara akavuka si mdogo sana kivile. kweli hasira hasara na hapa inatufundisha sisi wenye familia kuwa na kitu kinaitwa wosia baada ya kufa mali ziendeje ila my dear mama Malaika mwanaume ukimweleza habari hizi lol anakuona nuksi kweli wakati ni kwa faida yetu.

Comment by Mama Malaika on October 21, 2013 at 11:15
ANGELA.... wewe una mawazo mazuri. Families nyingi mtu akifa ndio matatizo yanapoanza ajili ya mali iliyoachwa na marehmu. Ni vyema kutafuta mwanasheria kuandika legal documents (Will) mtu ukiwa hai, siku ukifa ukishazikwa documents zasomwa hadharani (mahakamani) maagizo na majina yote uloandika kwenye documents ukiwa hai kuanzia mtu ulomchagua kulea watoto wako, mtu atayesimamia biashara zako, jinsi mali zitavyogawanywa na majina kuwa yanayoonyesha nani atayerithi nyumba, shamba, gari hadi vikombe na sahani. Maana kuna watu wanagombea kurithi hadi vyombo vya jikoni
Comment by Mama Malaika on October 21, 2013 at 10:36
- Asante Angela kwa ufafanuzi maana wengine tuko mbali. Huyo mtoto jamani naona kachanganyikiwa na ana majonzi sana kwani umri huo ana akili kutosha kujua nini kimetokea. Na yaelekea huyo bwana alikuwa na hasira sana hadi kurusha risasi ki-hivyo ndani ya nyumba, sasa hizo risasi zilizotoboa toboa nyumba si zingeweza penya na kumuua mwanae wa kuzaa?? Ama kweli HASIRA hasara.

- Dismas... Iwapo mtu kazamilia kujiua (na sio kujijeruhi), aweza jiongeza nyingine hadi pumzi ya mwisho inapoishia ukizingatia siku bunduki ndogo nyepesi.
Comment by ANGELA JULIUS on October 21, 2013 at 7:35

Mama Malaika mtoto alikuwa akilelewa na mama yake Ufoo ambaye sasa ni Marehemu. wachumba walikuwa wakiishi pamoja ila ndo hivo uchumba wa spaner mkononi.

kuhusu mali zao kiukweli huko siwezi sema chochote siku zote napenda kusema kitu nilicho na hakika nacho.

Na hata hao ndugu watakuwa wajinga kuingilia mali ya marehemu na Ufoo kwani Ufoo naye ni mfanyakazi na yeye kiukweli hayupo vibaya kuanzia familia yake.

Hapa ushauri wangu ndugu tusipende kuingilia mali za ndugu zetu wanapokuwa wameaga dunia kwani kama anayo familia ile ni mali ya familia yake unaingilia nini unajuaje walitafuta vp kiukweli watu wenye tabia ya kuingilia mali wakati mtu anapokuwa hayupo duniani as if wao wanaishi milele ni sawa na wauaji.

Comment by ANGELA JULIUS on October 21, 2013 at 7:29

Chikira ungekuwa karibu ningekupa zawadi lait angeanza na ya kidevu asingeweza kujipiga kwingine lakini kama alianza na sehemu nyingine ambazo si hatari hata kumi angejimiminia kama alivoharibu nyumba ya watu na matundu ya risasi jamaa alikuwa akizirusha mle ndani utafikili alikuwa akiua mbu lol inasikitisha sana kama mdau mmojawapo angefanikiwa kuwa eneo la tukio. kiukweli picha nzima ninayo Mungu ampe Ufoo Uponyaji akipenda kuadithia kiundani atasema kama alivoahidi kueleza atakapopona.

Comment by ANGELA JULIUS on October 21, 2013 at 7:26

mama Malaika mtoto wa marehemu aliyezaa na dada Ufoo ana miaka kama 9 hivi sipo sure sana na ni wa kiume.

@ mzee mwenzangu Manka siri hajafa nayo mtuhumiwa siri ipo ni kumwombea Ufoo apone then siri itajulikana kwani naye Ufoo angekuwa amekufa tungesema siri wanayo marehemu wote.

kiukweli marehemu mtuhumiwa alikuwa amejiandaa kwa kuua kwani kwenye gari lake vitu binafsi nilivoviona ni balaa anaonyesha alijiandaa haswa tena alisema alikuwa anataka kuua familia nzima.

Comment by Chikira Chikira on October 20, 2013 at 23:34

Pande zote wawe wavumilivu!! what is done is done!!

ila risasi kujipiga mara mbili inawezekana tu, inategemea risasi ya kwanza ilikuwa imepiga sehemu gani ya mwili na ilijeruhi kiasi gani, kujipiga mara mbili nikule kutimiza lengo la kile mtu alicho kusudia!!! kama umelenga kujiua na umejipiga yakwanza na kuona haijalenga ulichokusudia basi unaweza kurudia sehemu unayoona itakamilisha ulichokusudia!!!

Comment by manka on October 20, 2013 at 22:21
Siri amekufa nayo mtuhumiwa ' hivyo tumwachiw Mungu ahukumu kasiri ya mapenzi yake.
Comment by David Edson Mayanga on October 18, 2013 at 19:51

mh siri kubwa

Comment by CHA the Optimist on October 18, 2013 at 18:46

Vere vere kompliketed!

Ila acheni vyombo husika vifanye kazi yake, maana vyombo husika vina uwezo wa kubaini nini kweli na nini uongo!

Mungu awabariki wote.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*