Tulonge

Mtoto wa msanii Afande Sele ambaye uwezo wake darasani umemfanya aanze kidato cha kwanza akiwa na miaka 11

Afande Sele kulia, akiwa na mwanae Tunda

Wale wafuatiliaji wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' watakua wanamfahamu vizuri Tunda ambaye ni mtoto wa mfalme wa Rhymes Tanzania, Afande Sele. Tunda alipozaliwa takribani miaka 11 iliyopita, Afande Sele alikua akimtaja sana katika nyimbo zake na alipokua akihojiwa.Hii ilipelekea jina la Tunda kukaa vichwani mwa Watanzania hasa mashabiki wa Afande Sele.

Tunda huyu sasa ni binti wa miaka 11, na sasa yupo Kidato cha kwanza. Ni binti mwenye uwezo mzuri darasani. Alifanya mtihani wa Darasa la 7 kipindi alipokua darasa la 6 na kufanya vizuri. Hii ni kwa mujibu wa baba yake kama alivyoeleza hapo chini kupitia ukurasa wake wa facebook.

Hapa chini ni familia nzima ya Afande

Toka kushoto ni Tunda,Sanaa,Afande na Mkewe. Mambo ya nyota ya kijani umeyaona mdau?

Views: 2151

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on October 22, 2013 at 8:26
ndo inavyotakiwa tunda akaifanikiwa kimaisha atamlea mdogo wake bila shida yoyote tubadilike wa tz kuzaa si kazi kazi je mtoto atapata malezi yaliyobora na elimu bora?
Comment by Monica on October 21, 2013 at 19:09
Mizizi imefanya kazi,
Comment by Chikira Chikira on October 19, 2013 at 15:27

Hii ni zaidi ya nyota ya kijani naona!!!!!!

Comment by Mama Malaika on October 19, 2013 at 3:45
Nimeyaona Tulonge. Nimeipenda sana usia alotoa kwa mwanae Tunda
Comment by Tulonge on October 19, 2013 at 0:39

Mambo ya family planning umeyaona mdau?

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*