Tulonge

Songea: Mtoto wa miaka mitano akatwa panga mdomoni na usoni kwa kutuhumiwa kuiba mapera

KATIKA hali isiyo ya kawaida ambayo imewashangaza wakazi wengi Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, mtoto Benson Nilah (5), mkazi wa madizini katika manispaa hiyo amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa panga usoni na mdomoni mithili ya kibaka.

Mtoto huyo ambaye ameshonwa nyuzi sita na amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, anadaiwa kufanyiwa ukatili huo na mkazi wa Madizini, Ronginus Haule (50), akimtuhumu kuiba mapera kwenye bustani yake.

Tukio hilo la kusikitisha na ambalo limekuwa gumzo mkoani hapa, limetokea juzi majira ya saa moja jioni.
Benson ambaye ni mtoto wa pili wa mtangazaji wa Kituo cha Radio Maria Tanzania mkoani Ruvuma, Jofrei Nilah, anaendelea kupata matibabu akiwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU ).

Akielezea tukio zima, mama mzazi wa mtoto huyo, Rwosita Nyoni ambaye ni mke wa Nilah, alisema kuwa mtoto wake hakuwepo nyumbani tangu majira ya saa saba mchana, na alipomtafuta kwa ajili ya chakula cha mchana hakuweza kumpata hadi ilipofika majira ya saa moja jioni.

Alisema wakati anatoka kanisani, alikuta mkusanyiko wa watu wakimshangaa mtoto ambaye alikuwa hafahamiki wa nani ambaye alikuwa ameumizwa vibaya na kutapakaa damu mwili mzima huku akiwa amepoteza fahamu.

Alisema wakati akijishauri kusogea eneo la tukio, alikuja jirani yake ambaye alimtaja kwa jina la baba Said na kumshauri asogelee eneo la tukio huenda akawa ni mtoto wake, na aliposogea aligundua kuwa ni mwanae Benson jambo ambalo lilimshitua sana.

Kwa mujibu wa habari hizo, Nilah aliamua kwenda polisi ambako alipatiwa fomu namba tatu na kisha alimpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu ambako alipokelewa na kulazwa wodi namba tano.

Muuguzi wa zamu katika wodi hiyo, Erenesta Kapinga, alisema hali ya mtoto huyo ni mbaya na wamelazimika kumhamishia kwenye wodi ya wagonjwa mahututi kwa uangalizi zaidi.

“Tunahisi amehumizwa ndani kwa ndani na damu zitakuwa zimevujia kwenye ubongo, na sehemu za tumbo nazo atakuwa ameumizwa kwa sababu akikojoa anatoa damu, hivyo kwa sasa tunasubiri majibu ya X-Ray ili tubaini ameumia eneo gani,” alisema muuguzi huyo.

Mmoja wa wanaharakati wa kituo cha wasaidizi wa sheria wanawake na watoto mkoani Ruvuma, Fatuma Misango, ameelezea kusikitishwa na tukio hilo ambalo alisema kuwa ni la uuaji, kwani umri wa mtoto na adhabu aliyopewa haviendani.

Hata hivyo, mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Ruvuma (HOMSO), Dkt. Benedicto Ngaiza amethibitisha kumpokea mtoto ambaye amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa mapanga usoni, na kwamba kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu akiwa chini ya uangalizi maalumu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi, hakuweza kupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.
Chanzo: mdodosaji blog

Views: 1144

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Salim Nassor Rashid on December 2, 2013 at 13:27

PERA TU!!!!!! KWELI DUNIANI KUNA WASHENZI SANA. SHERIA ICHUKUWE MKONDDO WAKE.

Comment by ABRAHAM PONERA on November 28, 2013 at 12:48
mapera ukithaminisha na uhai wa mtoto huyo wapi na wapi? hayo ni manyanyaso viongozi washika dola wawatafute wahaini hao kwa nguvu zote
Comment by Hashim Said on November 25, 2013 at 18:54

Mmh!

Comment by Omary Maftuhi Mwinshekhe on November 25, 2013 at 12:16

Jamaa ametoa adhabu kubwa sana ukilinganisha na uzito wa kosa lenyewe.

Comment by Bonielly on November 25, 2013 at 11:45

unajua hizi ni hulka za watoo nakumbuka hata mimi wakati nasoma tulikua na katabia tukitoka shule tunaingia kwenye shamba la kanisa kulikuwa na matunda mengi sana tofauti, kulikuwa na walinzi basi tunawacheki walinzi na kuingia kuna siku wakatukamata tulitandikwa mikwaju ya maana, lkn kutokana na utoto hatukukoma, sio kama tulikuwa hatuli nyumbani na posho ya chakula tunapewa, sio ugumu wa maisha rahasha, nyingine hasira za mwenye shamba kila siku mapera yanaisha, ukiwaambia ndio kama umewatia pilipili, si unajua watoto tena,, 

Comment by Hellen Attarsingh Gupta on November 25, 2013 at 10:35

Jamaniiiiiiiii. Maperaaaaaaaa. Mapera tuuu? Au kuna jambo nyuma ya pazia?

Comment by MGAO SIAMINI,P on November 25, 2013 at 10:15

ugumu wa maisha umepunguza upendo

Comment by habiba mustafa mlawa on November 25, 2013 at 9:18
mapera tu ndo yanataka kutoa uhai wa mtoto, watu mbona siku zinavyozidi kwenda ndo wanakuwa na roho mbaya

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*