Tulonge

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo afanyiwa maombi ya nguvu

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake.

Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu.

Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Chanzo: MichuziBlog

Views: 798

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Hashim Said on November 26, 2013 at 20:53

Yaani badala ya kuiombea Tanzania iondoke gizni... eti viongovi wa madhehebu mbalimbali wanamuombea yule yule alotuweka gizani! Naungana na wadau CHA the Omniscient na Dixon Kaishozi.

Comment by Dixon Kaishozi on November 24, 2013 at 15:21
Pongezi kwa nchi kua gizani kwa zaidi ya saa 24.. sijawahi ona mgao kama huu unaoendelea.
Comment by CHA the Optimist on November 22, 2013 at 18:20

Unafiki, unafiki, unafiki kila kunapokucha hapa Tanzania. Mbaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa kidini nao ni wanafiki! Ni lipi la kumpongeza huyu Peter Muhongo?

Tuache tabia za kujipendekezapendekeza jamani.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*