Tulonge

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mwanza auawa na wananchi

Taarifa zinasema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu, Mhe. Clement Mabina  ameuwawa na wananchi wenye hasira kwa kupigwa na mawe na silaha za jadi mwendo wa saa 2 asubuhi katika kijiji cha Kanyama.

Imeelezwa kuwa chanzo cha shambulio lililomuua Mabina inatokana na ugomvi wa ardhi ambapo kesi ya eneo hilo ilikuwa ikiendelea mahakamani, lakini mchana wa leo, marehemu Mabina alionekana akipanda miti na kuweka mawe ya msingi katika eneo lenye ugomvi na wananchi walipomhoji kuhusu kibali cha mahakama cha kufanya hivyo, inaripotiwa kuwa aliwatolea lugha chafu na kuwatisha kwa bunduki ambapo alifyatua risasi ili kuwatawanya.

Inaripotiwa kuwa moja ya risasi iliyofyatuka ilimpata mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kumsababishia mauti. Baada ya risasi kuisha, ndipo wananchi walimzingira, wakamvamia na kumpiga kwa silaha mbalimbali ikiwemo mawe, mishale, mikuki na mapanga hadi kumsababishia mauti.

Kabla ya kurejea CCM, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.

Mabina pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.

Mwaka 2012 akiwa CCM, aligombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama ngazi ya Mkoa wa Mwanza lakini alishindwa na aliyewahi kuwa Waziri na Mbunge wa Ilemela Dk Antony Diallo.

Taarifa zaidi zitapatikana kwenye vyombo rasmi vya habari hapo baadaye.

Maelezo na wavuti.com

Views: 1593

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 19, 2013 at 16:29
Asante sana Dixon. Hiyo ndio Tanzania watu wanayoambiwa imejaa amani huku viongozi wana uwezo wa kuzulumu ardhi ya wanyonge. Imefikia kipindi nakata tamaa na nyumbani
Comment by Dixon Kaishozi on December 17, 2013 at 9:28

Pole sana Mama Malaika.. ila wanacho kitafuta ni kama cha huyu bwana.. Watu Wakisha choka kifuatacho ndiyo kama hicho!!! Pole sana, vyote ni vyakupita. Aridhi hii tunayopigania mwisho wake itatufukia tu!!! 

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 12:46
Hii wala sishangai. Hata mie nimeshakumbwa na mkasa wa kunyang'anywa ardhi/shamba sehemu mbili tofauti. Tena shamba moja lilikuwa la urithi, roho yaniuma hadi hivi sasa 2013 bado sina raha nikifiria. Nimeshuhudia wana kijiji wamenyanganywa mashamba/ardhi kwa nguvu bila fidia ambayo walikuwa wakiishi na kutegemea lisha families, na ardhi hiyo kulikuwa na makaburi wamezika wapendwa wao. Nchi ilipofikia ni pabaya sana.....
Comment by Hashim Said on December 16, 2013 at 11:06

Siku zote usibishane na nguvu ya umma! Hutowaua wote hata kama silaha ya moto!

Comment by Dixon Kaishozi on December 16, 2013 at 10:17

Hiyo ndiyo nguvu ya uma!! Alitaka kutumia ubabe matokeo yake ndiyo hayo.. Kaua na yeye kauliwa.. malipo ni hapa hapa duniani. Kwa upande wangu siwezi shiriki kutoa mtu roho.. ila simuonei huruma hata!! Hawa jamaa wanaona nchi ni yao.. cccm!!! NAAMINI SIKU WANANCHI WAKICHOKA - HATA MJE NA VIFARU.. HIKI NDICHO KITAKACHO TOKEA!!!!

Comment by Omary on December 16, 2013 at 9:59
Doh! yaani watu wamechoka kiasi hiki? mwenyeziMungu tusaidie ndio dhuluma sio nzuri ila kuutowa uhai wa mtu nao sio kazi ndogo sijui hawa watu wzna roho za aina gani?
Comment by ANGEL NEHEMIAH on December 16, 2013 at 9:33
Mh! Hata sijui niseme nini? Tunakoelekea ni giza nene.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*