Tulonge

Majambazi 7 yambaka mama na mabinti zake watatu kwa zamu huko Geita

Watu  wanaokadiriwa kufikia saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na mapanga na marungu, wamevamia nyumbani kwa mkazi wa kijiji cha Kaduda kata ya Katoro wilayani Geita na kuwabaka kwa zamu mama na wanawe watatu kwa zaidi ya saa mbili.

Hali kadhalika, watu hao walimjeruhi mmoja wa watoto wake wa kiume aliyekuwa akishuhudia unyama huo ukifanyika.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 15, mwaka huu baada ya kuvamia na kuvunja mlango wa nyumba walimokuwa wamelala wakati baba mwenye mji huo akiwa safarini.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Jumanne Faida, alisema baada ya kutekeleza ukatili huo, mama na watoto hao walipiga yowe kuomba msaada.

Faida alisema kuwa watu hao walikuwa wakimbaka mama huyo na wanawe hao wenye umri wa kati ya miaka 14, 10 na 17 kwa kupokezana mbele ya mtoto  wa kiume ambaye walimjeruhi kwenye paji la uso kumcharanga kwa panga.

Mganga wa zamu wa Kituo cha Afya cha Katoro, Dk. Daneil Izengo, alithibitisha kuwapokea mama na watoto wake hao kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi na wa kiume kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, hakupatikana   kuzungumzia tukio hilo.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omary Mangochie, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema polisi walikuwa hawajamfahamisha rasmi.

Hata hivyo, Mangochie aliahidi kufuatilia ili waliohusika wasakwe na kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

 

via: mdodosajitz.com

Views: 451

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on December 23, 2013 at 11:50

'Tanzania ni kisiwa cha amani' kiukweli nikisikiaga maneno haya navurugikiwa akili hasa yakitoka midomoni mwa watawala

Comment by Mama Malaika on December 19, 2013 at 16:13
Inatisha na kutia huruma. Halafu viongozi wakipanda majukwaani wanahubiri kuwa Tanzania imejaa amani.
Comment by ANGELA JULIUS on December 19, 2013 at 16:09

KWA JINSI NILIVOISOMA HII HABARI HAWA WALA HAWAKUWA NA HAJA YA KUIBA CHOCHOTE WALIKUWA NA HAJA YA KUTENDA HUU USHETANI WAO TUU NA WAKIFIKIRI LABDA WANGEMKUTA BABA MWENYE NYUMBA ILI AONE JINSI WANAVOMFANYIA MKEWE NA WATOTO WAKE.

Comment by ANGELA JULIUS on December 19, 2013 at 16:06

MH KWELI INATIA HURUMA NA SIMANZI SANA MUNGU WA KISASI ATATENDA KAZI YAKE SAWA NA MAPENZI YAKE AMIN

Comment by Dixon Kaishozi on December 19, 2013 at 9:17

Dah!!! Inatia huruma sana!! Viongozi wako wapi kuwalina na kuwatetea raia wao? Mwandishi wa habari anapata taarifa alafu kiongozi husika eti anasema hajui lolote!!!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*