Tulonge

Yule mkalimani 'fake' wa mazishi ya Mandela alazwa hospitali ya magonjwa ya akili

Thamsanqa Jantjie, mkalimani wa lugha ya ishara

Mkalimani wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya akili.

Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.

Thamsanqa Jantjie "anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.

Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi mbalimbali wakitoa hotuba zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson Mandela wiki iliyopita.

Bwana Jantjie amesema aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia.

Amesisitiza kuwa alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.

Chama tawala cha African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.

Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.

BBC Swahili

Views: 432

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on December 23, 2013 at 11:34

UMARUFU KAZI JAMAA KASHATOKA ASINGEKOSEA ASINGEJADILIWA DUNIA NZIMA

Comment by ANGEL NEHEMIAH on December 23, 2013 at 9:40
Hahaha! Kaazi kweli kweli.
Comment by Mama Malaika on December 20, 2013 at 15:18
Ha haaaa haaaa.... Mjini shule @ Angela. Anatumia ugonjwa kama kinga baada ya kubanwa na wananchi wa South Africa wakitaka arudishe pesa aliyopewa na vigogo wa ANC.
Comment by ANGELA JULIUS on December 20, 2013 at 12:48

Mh changa la macho ina maana alipokuwa pale anaonyesha hizo maana za lugha ndo kilikuwa kinamuanza? mbona hajasahau kuvaa nguo na mambo mengine. hii sababu ya yeyey kulazwa hosp ni janja tuu ili ionekane ugonjwa ndo ulikuwa unaanza.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*