Tulonge

Kazi kwenu, Rasimu ya katiba mpya hii hapa


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete aliitaka Tume hiyo ya Katiba kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo inawekwa kwenye mitandao yote ya kijamii ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandaoni.


Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.Jaji Warioba alisema kuwa kulingana na idadi ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu waliohitaji Serikali tatu kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuundwa mapema mwezi Januari mwakani.
Bofya hapo chini ili kuishusha Rasimu ya katiba mpya

Chanzo: Issamichuzi Blog

Views: 589

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on January 2, 2014 at 23:13
Ha haa haaaa... CHA. Ujue faida kubwa ya "Dual Citizenship" ni uwezo wa Tanzania diaspora kuwa huru ku-register na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu Tanzania bila kujali mtanzania huyo ana uraia wa Britain alikosoma na kupata kazi. Na hiyo ndiyo moja ya vigezo ya Katiba mpya ya jirani zetu wakenya (2011) kuruhusu "Dual Citizenship". Na hii iasaidia wasomi (Tanzania Diaspora) kuwa na uhuru na moyo wa kuingia Tanzania bila vikwazo hasa kwa lecturers, doctors, etc. wanaopenda kutumia likizo zao as a voluntary work hasa hospitals mikoani ambako kuna upungufu wa watalaamu bila kuomba Tanzanian working visa kwenye ubalozi kama ilivyo sasa.
Comment by Mama Malaika on January 2, 2014 at 22:55
Kwa mie "Dual Citizenship" ni kwa ajili ya watoto wangu hapo baadae @ CHA the Omniscient. Kwa mtoto anayezaliwa na wazazi toka nchi mbili tofauti, identity yao iko very fluid. Citizenship ndio identity kubwa mtoto wangu atayojivunia kuwa yeye ni mtanzania na sio kupitia ancestors. Mfano mzuri ni jirani zetu wa Kenya na mtoto wao mashuhuri Barack Obama (raisi wa US). Soma vitabu alivyoandika Obama, kuanzia "Dreams From My Father" cha 2004 na "The Audacity of Hope", hutokuta sehemu hata moja kaandika kuwa yeye ni Kenyan, asema kuwa yeye ni American aliyezaliwa toka kwa 'black African father from Kenya and a white American mother'.
Comment by CHA the Optimist on January 2, 2014 at 18:55

Ha ha ha ha! Mama M, na Eddie naona mnashupalia sana uraia wa nchi mbili (dual citizenship)--hilo mimi kwangu si tatizo, na nina imani mambo yatakuwa mazuri.

Mimi kwa maoni yangu na ningekuwa na uwezo, ningeamua kuwe na serikali moja tu. Hii itapunguza gharama za kuendesha serikali ambazo kiukweli zitakuwa kubwa mno.

Haya mambo ya Serikali tatu kwa kweli, tujiandae kukamuliwa sana.

 

Comment by Mama Malaika on January 2, 2014 at 18:33
Kaka Eddie nami leo asubuhi nimesoma hadi page 58 kujua Katiba mpya yasemaje kuhusu "Dual Citizenship" bado sijaipata uzuri kwani kwenye "Sura ya Tano" (pg 22-3) ambayo inahusu "URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO" kuna kifungu cha mwisho (page 23 kwa chini) kina elezea "Hadhi ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania", nacho kimeandikwa hivi:

59. Bila ya kuathiri masharti yaliyomo kwenye Sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.
Comment by Mama Malaika on January 2, 2014 at 18:24
Bofya hapo chini mwisho wa blog ku-download (PDF file) ili uweze soma ni pages nyingi (118). @ kaka Eddie
Comment by eddie on January 2, 2014 at 14:56

Dual Citizenship wameamua vipi?

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 2, 2014 at 10:46

NA MIMI NAITAKA TANGANYIKA JAPOKUWA ILIKUFA KABLA SIJAZALIWA MIUNGANO YA KISANII HATUTAKI

Comment by Abasi Mikidadi on January 2, 2014 at 10:01

TANGANYIKA YETU ILEEEEEEE YAJA

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*