Vikundi vya kutetea haki za binadamu Angola vilikuja juu kufuatia onesho alilofanya mwanamuziki maarufu Duniani Mariah Carey kwa ajili ya Rais Josè Eduardo Dos Santos kwa muda wa masaa mawili na kulipwa dola milioni 1 ambazo ni sawa na sh. bilioni 1.6 za Kitanzania. Onesho hilo lilifanyika katikati ya mwezi desemba mwaka huu kabla ya xmas.
Vikundi hivyo vimemlaumu Rais kwa kuendekeza anasa wakati wananchi wake wengi wanaishi maisha duni. Pia amekua akishutumiwa kwa kuwaua wanasiasa, wanaharakati na viongozi ambao watakwenda kinyume na msimamo wake hata kama haufai.
Rais Dos Santos kulia akiwa na familia yake pamoja na Mariah Carey(mwenye gauni jeupe katikati)
Add a Comment
Mh......naomba nirudi kuchangia nikiwa nimelewa pombe. Maana nikichangia kwa akili yangu ya kawaida, kuna mengine naweza nisiongee kutokana na aibu wakati ni lazima niyazungumzie.
Huo ni ubadhirifu wa mali ya umma!
'upolaji wa mali ya umma' Hawa viongozi wa Afrika wana...........malizieni wasiopenda mtindo huu
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge