Tulonge

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule

Via: Jamii Forum

Views: 2152

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 28, 2014 at 18:10
Narudia tena... kuna swali naomba jibu.. kitimoto imeshauriwa tuiache.. sawa!! NIMEJIULIZA INA MAANA MAZIWA NA NYAMA NAVYO TUSITUMIE kwa kile nilichokieleza hapo juu?
Comment by Mjata Daffa on January 28, 2014 at 17:41

Zainabu ngoja nikakutafutie AYA kwenye Bible, halafu tuendelee na mjadala maana wewe unaonekana unapenda ushahidi. lakini umeshawahi kusoma BIBLE? nisijekupa aya ukaikataa

Comment by Dixon Kaishozi on January 28, 2014 at 16:56

Pamoja sana  sis Zainabu, Ndugu CHA asante kwa kupigilia mstari.. teh teh na Sitaki kukupinga ndugu yangu Mjata!!!  na kufanya kama "Malumbano ya hoja.. hehehee" ila tu kuwa profesa, dokta na vitu kama hivyo haimaanishi wao ndiyo tukubaliane nao kwa kila kitu!! Angalia wanao itwa.. WAHESHIMIWA... wengi wamepewa huo udokta na uprofesa wa kuunga unga!! na wao waje waseme kitu nikubaliane nao moja kwa moja ?

Kuna ugonjwa unaitwa  BRUCELLA - kwakifupi unapatikana hasa kwenye maziwa na nyama!! upande wa maziwa hasa ya mbuzi.. na kwa upande wa nyama ni hasa hizi nyama choma!!

Ndiyo maana nilitoa hitimisho kwa kusema hivi"chakula chochote, kisipo andaliwa vizuri huleta madhara na nyama ikiwa mojawapo"

 

Nadhani nimesomeka!!!

Comment by CHA the Optimist on January 28, 2014 at 16:40

Ha ha ha! Mgongano wa Mawazo between Mjata, na Dixon......yap hatuwezi kukubaliana kwa kila jambo. Lazima tuwe na tofauti hata kama tumezaliwa toka baba na mama mmoja.

Ila hapa ni mahala pa amani.

Big Up Dixon kwa kuwa mbishi, Big up Mjata.

Comment by CHA the Optimist on January 28, 2014 at 16:32

Haya mambo ni magumu sana.....tatizo hii dunia ukweli unaweza geuzwa kuwa uongo na uongo unaweza geuzwa kuwa ukweli. Inahitaji udadisi sana wa mambo kujua ukweli angalau unaweza kupata mwanga. Maana most of us tuko gizani, na mbaya zaidi we have been brainwashed into believing that whatever the Professors (the wasomi) say, is true without asking.....why is it true? Professors are just human beings, they sometimes lie, just as those who are not professors do. They say truth, just as those who are not Professors do. They forget, just as those who are not professors do. They are not angels that we have to agree with them in everything what they say or do.

Ila kuna sehemu katika Bible........Mark 7:15-20.............. inasema...

"There is nothing outside a person that by going into him can defile him, but the things that come out of a person are what defile him.” And when he had entered the house and left the people, his disciples asked him about the parable. And he said to them, “Then are you also without understanding? Do you not see that whatever goes into a person from outside cannot defile him, since it enters not his heart but his stomach, and is expelled?"

Ndio maana nasema haya mambo ni magumu. Yahitaji udadisi wa hali ya juu kujua facts.

Nimalizie tu kwa kusema...yawezekana Mjata Daffa yuko sahihi, inawezekana Dixon yuko sahihi, inawezekana Utafiti huo ni sahihi pia.

Kikubwa ni kuwa na udadisi. Kila tunachokiona ni vizuri ama tujenge tabia na tamaduni ya kujua ukweli ama undani wake. Tusiwe wepesi wa kukubali kila tunachoambiwa--lazima tuhoji. Tusiwe wepesi wa kupinga kila tunachoambiwa, lazima tudadisi kwanza.

Comment by Zainabu Hamis on January 28, 2014 at 15:26

Aya Mjata Daffa

Comment by Mjata Daffa on January 28, 2014 at 8:46

Kwa sababu mimi na wewe ni wavivu wakusoma ndio maana unauliza kama hilo "which part in the Bible" nakushauri kama unaishi na msabato karibu ambae anaiamini BIBLE kama wewe muombe akuonyeshe hilo andiko hi. Pia hujakosea kuwa upande wa DIC kwa sababu watanzania tunauhuru wa kuamua ili mradi usivunje sheria. unakumbuka maneno ya mzee RUKHSA? Namnukuu ukitaka kula chura, Panya, NGURUWE au Nyani Rukhsa.

Comment by Zainabu Hamis on January 27, 2014 at 20:50

Tusikubaliane tu na utafiti wa the so called Profesa. Yeye si Malaika kuwa kila anachosema ni sahihi. Kuna mengi sana tunadanganywa. Dixon I am on your side.

Comment by Zainabu Hamis on January 27, 2014 at 20:48

Ooooops! Mbona mnaniacha njia panda. Which part in the Bible....forbids NGURUWE Bwana Mjata?

Comment by Mjata Daffa on January 27, 2014 at 9:11

Kaka DIC, nakushauri kuaacha tu, hamna njia nawala usimzalilishe PROFESA kwa sababu ya tamaa binafsi mpaka amepata uprofesa maana yake dunia imemkubali kwa tafiti zake iweje wewe mwenzangu mimi umkosoe? angalia usije ukawa wewe ndio umekurupuka mkuu.

OK achana na huyo profesa MUNGU nae alikurupuka kwakutaza Nguruwe kwenye BIBLIA NA

QURUAN? lengo la Profesor ni zuri na amekusudia kukusaidia wewe na watumiaji wengine wa ngurue. BIG UP PROF!!!

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*