Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya chama hicho huko Mbeya jana.
Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya
JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.
Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.
Chanzo: Michuzi Blog
Add a Comment
Uzalendo ni mgumu sana
nahisi labda jina langu lilijificha kwenye neno (na wengine wote) kilichoniuma kwanini ulimtaja angela mimi haukunitaja bora mimi na angela ungetuweka humo ndani, kwa wengine wote! aksante kaka dicked kwa kwa kaubagizi kako na wewe hujamtaja angela,
Asante Dixon kwa kunisaidia. Maana Bonielly asingeniamini. Yaani sijui kwa nini Admin ali-delete jina lake kwenye maoni. Ha ha ha ha!
Bonielly, sijui hata ilikuaje? Nilikuorodhesha na wewe katika maoni yangu ya awali, sasa sijui Admin (Dismas) amefuta kwa sababu zake anazojua, yaani ndo nashangaa sasa kutokuliona jina lako wakati niliorodhesaha. Tehe tehe tehe!
Kwanza nasikitita (cha) kunitenga bila ya kutaja jina langu na kumtaja angela, au sina haki ya kupenda chama? kwanini usinitaje bwana cha? haujui kama mimi na angela ni mapacha? usirudie tena siku nyingine, (NI UTANI TU) Unajua zipo stail za kujiunga na chama lkn sio hizi stail, zinaonesha kama ni usanii kwamfano, kama alivyosema bro dicked, kutoka dar hadi mbeya, je dar hawawezi kujiunga? (2)kwenda kundi zima kwa pamoja, je waonekane kwa rais? (3) siku zote walikuwa wapi? kwa kweli wachangiaji mliopita nimewaelewa, mimi mtazamo wangu, namuachia mungu,
Dix atakae kuchukia hajui maana ya democrasia, uko huru kusema unavyofikiri bila ya kuingilia uhuru wa mwinzio. BIG UP,
Lakini nakukumbusha kido msanii kujiunga na CCM siojambo geni, Hadija Kopa, Viki Kamata, Asha Baraka na wengine wengi walijiunga CCM na mpaka leo wako CCM tena wamekua viongozi.
Swali? hawajamaa umewaita mambulula kwa sababu wamejiunga na CCM? AU kwa sababu waingia kwenye siasa? maana kama nikuchanganya siasa na usanii ungeanza kumhoji Professor J alipojiunga na CHADEMA Last year.
ilakama nikuichkia tu CCM utakuwa sahihi kuwaita hawa jamaa Mambulula.
Hawa ni mambulula.. sorry kama nitakua nimemkwaza mtu!.. Hapo wapo kwa masilahi zaidi.. Natolea mfano kwa msanii mmoja tu!! kwa wale waliopata nafasi ya kukumbana na tangazo moja alilocheza BABANA kupinga haya madudu ya serikali ya cccm inavyofanya Basi KAMWE HASINGEWEZA WEZA KUCHUKUA KADI NA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO!!!
Walikua wapi siku zote? kuchukua kadi ilisubiri kwenye sherehe zilizofanyika mbeya ? wote wanatokea dar.. kwani kule dar kadi ziliisha ? huko ni kujitafutia umaarufu usio kuwa na tija.. na kama mwenzangu alivyosema hapo chini.. Kipindi hiki watatumika sana.. Kuna mahali nilisoma mgogoro ulio kwenye chama cha bongo movie kuhusu kupokea pesa ili wajiunge na chama tawala ambapo imepelekea mwenyekiti wao Steven Nyerere kuambiwa ajiuzuru..
Hamna kitu hapo!!! Msinichukie jamani na mimi ni mtazamo wangu tu!!
Hao woote wapo hapo kisanii zaidi,ngoja watumike kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao then tutasikia mapya juu yao.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge