Tulonge

Obama atishia kusitisha uhusiano na Uganda endapo itapinga ushoga

Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika.

Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.

Marekani ni mojawepo wa mataifa ya kigeni yanayotoa kiwango cha juu zaidi cha msaada kwa Uganda, na mwaka 2011 idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani walitumwa kulisaidia jeshi la Uganda kupanda na kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA.

Lakini Rais Obama amesema uhusiano huo unaodhaminiwa sana utatatizika zaidi iwapo mswada huo wa kupinga mapenzi ya jinsia moja utaidhinishwa na kuwa sheria.

Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani, Susan Rice, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba amefanya mazungumzo ya kina na rais Museveni jumamosi usiku kumtaka asitie saini mswada huo.

Mbali na Uganda rais Obama amelalamika kwamba visa vya mashambulizi na kuhangaishwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja vimeenea katika mataifa kadhaa kutoka Urusi hadi Nigeria.

BBC Swahili

Views: 1457

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by chaoga on February 28, 2014 at 15:36
Comment by CHA the Optimist on February 27, 2014 at 19:38

Chaoga No, No, No, No. I say Noooooooooo!

Comment by chaoga on February 27, 2014 at 18:16

CHA Nakujibu hivi....

hapo umezungumzia utamaduni nazani hujazielewa nchi za magharibi kwenye hili suala la ushoga wao wamezama kabisa kwenye HAKI ZA BINADAM, Kila binadam ana haki ya kufurahia maisha bwana badilika mkuu ILA SIE WAUMINI WA UTAMADUNI NA WA DINI TUJITAHIDI KUELIMISHA VIJANA WETU KUHUSU HILI SWALA LA USHOGA. ILA MTU AKIWA TEYARI YUKO KUNDINI HUMO BASI TENA TUMKUBALI KWENYE JAMII

Comment by CHA the Optimist on February 27, 2014 at 15:58

Valued Relationship can never be sustainably maintained by one society being subservient to another Society---Yoweri Kaguta Museveni.

If you take men and lock them in a house for five years, and tell them to come up with two children, and they fail to do so, we'll chop off their heads. This thing seeks to destroy our lineage by saying John and John should wed, Mariam and Mariam should wed.---Robert Mugabe.

Kauli za Mugabe na Museveni kwa maoni yangu ni kauli za kuungwa mkono na kila Mwafrika wa bara hili la Afrika. Haiwezekani mimi CHA niwe na uhusiano mzuri na Angela JULIUS, halafu Angela anataka mimi tu nimsikilize na kumheshimu yeye. Ila yeye hataki kunisikiliza na wala kuniheshimu mimi. Hii si sahihi hata kidogo. Obama anadai kuwa uhusiano utayumba (na teyari umeshayumba). Mimi  nasema ni better kwa uhusinao kuyumba hata kuharibika kati ya nchi zetu za Afrika na nchi zao za Magharibi, kuliko uhusiano wetu uimarike wakati tamaduni zao tena zisizofaa mbele za Mungu zitawale kwetu, I say no to Obama and his companions.

I do plead all African leaders to follow in Museveni's footsteps, just to show them we are able to do our things, and we want to live the lives we want ili kudumisha na kulinda tamaduni zetu. Hata kama tamaduni zetu kwao ni za kishenzi, na sisi pia tunaona za kwao ni za kishenzi pia ndio maana hatuzitaki. Marcus Garvey aliwahi kusema "a man without history is like a tree without roots" sasa Obama na wenzake wanataka kupoteza kabisa roots zetu kwa ku-introduce ya kwao--No, No!!! Obama alikuwa moja ya wanasiasa ambao nimetokea kuwahusudu sana, lakini kutokana na hili la kutaka kuingilia mambo ya ndani ya nchi zingine hasa za Afrika nyumbani kwa baba yake, katika swala la tamaduni, nimeshamtoa katika list ya watu ambao ni wanasiasa ninaowahusudu.

Ehe, na mimi nimeandika kama gazeti la Mzalendo---ha ha ha ha ha ha! Ila Mama Malaika ndio kiboko. Akiandika yeye, ni Three in One yaani Mzalendo, The Guardian, na  The express.

Jamani, waafrika ni  lazima tuwe imara--tusiwaogope hawa jamaa. Ujasiri wa Museveni uwe mfano mzuri wa kuigwa na wote Afrikan Lidaz! Tukiwa wote sawa kwa hili, hawawezi kutuogopesha "NYAU" na watatuheshimu.

Comment by Omary on February 23, 2014 at 3:46
Mkuu CHA the .... pls nitafute kwa omaryngole@hotmail.com ninashida na wewe
Comment by CHA the Optimist on February 19, 2014 at 14:57

Ha ha ha! Nacheka kuongeza siku za kuishi.

Comment by chaoga on February 18, 2014 at 13:14

NASIKIA MUSEVEN KISHASAINI MUSWADA NA KUWA SHERIA SASA, NGOJA NIMPIGIE MSHKAJI WANGU OBAMA NIMWAMBIE ASITISHE SASA HIVI MISAADA YAKE UGANDA TUONE SASA NANI ATANUFAIKA NA HIYO SHERIA KATI YA MASHOGA AU WANANCHI KULALA NJAA MWISHOE SASA WATAZALISHA MASHOGA WENGINE (MWENYE NACHO ATAMRUBUNI ASIE NACHO ha ha ha ha ha )

Comment by Mama Malaika on February 18, 2014 at 10:59
Lol... Chaoga
Comment by Tulonge on February 17, 2014 at 16:26

teh teh teh Chaoga

Comment by chaoga on February 17, 2014 at 13:19

HATA MIE NAMUUNGA MKONO MHESHIMIWA OBAMA KILA MTU ANA HAKI YA KUPATA RAHA DUNIANI.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*