Tulonge

Mambo yameanza Uganda: Benki ya Dunia 'yaibania' msaada wa dola milioni 90

Wafadhili wakatiza misaada Uganda


Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .

Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.

Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.

BBC Swahili

Views: 783

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on March 1, 2014 at 16:40
Yaani we acha tu Chaoga, wanakuja na private jets zao kutua Birmingham airport siku za mashindano ya kimataifa ya mbio za farasi (Derby Racing) ambazo hushirikisha farasi wa wafalme na matajiri toka pande zote za dunia, ikifika jioni wanavyokunywa pombe na kufanya sodoma utasema sio wale uliowaona mchana wanaenda iwanjani wamevaa kanzu nyeupe na malemba yao kichwani. Waingereza wenyewe hawaingii kwa waarabu kwa sodoma na ulevi
Comment by chaoga on March 1, 2014 at 13:57

ni kweli mama watakaoumia ni wenzangu na mie tu, hao waarabu ndio usinambie kabisaa siwaamini hata kidogo naona hapo uingereza wanaponda raha tu...

Comment by Mama Malaika on March 1, 2014 at 13:23
Na kwa nchi za Africa, sheria nyingi zinabana baadhi kwani kuna watu Africa wako above the law. Sheria itawabana mashoga baadhi tu, mashoga matajiri (mapapa) wataendelea na vitendo hivyo bila shida. Hata huko kwa waarabu nchi zao ambako wana sheria kali ya vitendo vya ushoga, matajiri wa kiarabu na watoto toka the Saudi royal family wanafanya ushoga na wanaachiwa. Tena wanafanya mengi hadi na ulevi wa pombe na madawa ya kulevya hawashtakiwi, ila raia wa kawaida Saudia, Oman, etc. afanye hivyo atajuta kuzaliwa.
Comment by Mama Malaika on March 1, 2014 at 13:01
Nawaonea huruma walalahoi wa Uganda. Museveni na genge lake wana hela kibao na utajiri mwingi nje. Museveni akiumwa haendi India, apanda ndege kwenda west kwa matibabu (US, Britain, Germany, etc.). Wenzangu mie walalahoi ambao ndio asilimia kubwa ya population wanaitegemea hospitals za mikoa sijui taifa (Kampala) zinazotegemea vifaa vya misaada na budget ya sirikali na wizara ya afya ambayo ina miradi ya wafadhili (wa mama wajawazito, malaria, dawa kuongeza nguvu wagonjwa wa ukimwi, etc.) ndio watao athirika na hii issue. Na ndivyo ilivyo kwa Mugabe (Zimbabwe) kwenye hospitals imefikia hata drips kuwekewa wagonjwa shida zinaingizwa kwa magendo toka South Africa. Mugabe na genge lake wanatbiwa UAE, China.
Comment by chaoga on March 1, 2014 at 12:29

teh teh teh na viongozi wetu walivyo wa roho wa money watalegea wenyewe tu ...

Comment by Mjata Daffa on March 1, 2014 at 9:53

kaza BUT museveni usitishike bora kula nyasi kuliko kuuza uhuru wako

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*