Afisa Linda Okello akiwa kazini
Afisaa mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo kubwa.
Alipigwa picha akiwa amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.
Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana. Nini Kauli yako?
Chanzo: BBC Swahili
Chini ni picha ya askari huyo iliyosambaa kwenye mtandao wa whatsapp
Add a Comment
mmmmmmmmmh kweli yuko kikazi zaidi ila sio kazi ya uafande
Jamani dada huyu mbona akiuke maadili ya Jeshi la Polisi na bado asiadabishwe?
kiukweli kapendeza sana ila kwa mavazi ya watumishi wa Umma hilo haliruhusiwi angesubilia appointment zake na afande manyusi wa kiembe samaki ndo atinge. but all in all figure ipo bomba big up na pia she is natural on her body colour.
Alikuwa Kikazi Zaidi.....
Hahahahaaaa @ Dunda
Afande katokelezea na mungu kamjalia si utani mpaka unatamani uwe muarifu alafu yeye aje kukuarrest
Kwakweli alikuwa anatega watu.. ila sema wamemshadadia lakini ni kawaida.. Kapendeza mwenyewe .. hahaha.. Wivu tu !!!
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge