Tulonge

Ama hakika hii ndio tanzania tunayosema inaamani na kuheshimu haki za raia,ebu angalia hawa askari wakimsurubu kijana huyu ambaye si kibaka bali ni raia mwema tu ,lkn kwasabau wao wanazozijua wakampa…

Ama hakika hii ndio tanzania tunayosema inaamani na kuheshimu haki za raia,ebu angalia hawa askari wakimsurubu kijana huyu ambaye si kibaka bali ni raia mwema tu ,lkn kwasabau wao wanazozijua wakampa kosa la kuwakimbia na pikipiki wakati wakimsimamisha barabarani,lkn si kweli kijana huyu ni muuza maji na juice kwenye kituo cha basi,hata ilo pikipiki hajui.

Lkn ndio hivyo wameshaamua kutoa kichapo hicho,sasa tujiulize mimi na wewe mwanatulonge kuna haki hapa  na hiyoo amani wanayohubili kila kukicha hiko wapi.

Inasikitisha kuona mtanzania akinyanyaswa kwa kosa ambalo hakufanya bali amefananishwa tu na mwingine.Ni wangapi wameonewa,wamenyanganywa mali na wana usalama wa bongo,binafsi kikufurahishwa na nimeumizwa na kitendo hiki.

Views: 578

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on December 15, 2011 at 19:09

Ndio hivyo Mama...asante inatia huzuni sana vifo vya hao vijana wa Senegal.

Comment by Mama Malaika on December 15, 2011 at 18:58

Ujue huu uonevu wa polisi juu ya wananchi nchini Tanzania mie ndio kitu chanikera sana, mapolisi wanapiga raia na wakati mwingine kuwaua pasipo hatia yeyote ile. Natumai siku moja utasikia wananchi watamshika police na kumtundika makonde, nyie subirini.

@ Baraka... poleni sana na mauaji huko kwenu, niliona kwenye news.

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on December 15, 2011 at 14:26

Mkuu Bonielly...yaani we acha tu! Hatuna thamani kabisa sisi weusi, tena wakati mwingine tunadharauliana sisi kwa sisi na kujali wezetu, we angalia ukitaka kwenda kwenye manchi yao unavyosumbuka na kusaka kupata Visa, lakini wao wanapewa wakifika Airport Visa kuingia kwetu, huwa nakasirika sipati jibu kwanini tunawathamini sana hawa Jamaa zetu weupe na kuwa tetemekea sana. Tena kama hapo kwetu Bongo Airport, ukifika wewe Mtanzania kabisa nchi yako...unavyopelekeshwa kwa maswali mengi na vitisho vingi, lakini cha kushangaza unaona Wazungu wao wanapita tu bila wasiwasi wala kuuliza kitu....hivi kweli ni haki?

Comment by Bonielly on December 15, 2011 at 13:49

hapa kwetu juzijuzi kauawa mmama wa kichina na majambazi, yani mpaka mawaziri wamechanganyikiwa, leo auwawe mtaliano hapa uangalie huo msala wake, lkn sisi weusi thamani yetu iko wapi? mungu saidia,

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on December 15, 2011 at 13:37

Poa Mkuu Gratious, hata mimi imeniuma sana tena sana tu! nchi kama Italia bado inakuwa na watu wabaguzi kiasi hiki...yaani sijaamini kabisa, sikutegemea kabisa. Yaani amewauwa jamaa hawana hatia yoyote kabisa, kwasababu zake hizo za kishenzi tu, kwasababu ya kuchukia weusi tu....yaani kitendo hiki sijakubaliana nacho kabisa, kitanifanya nirudi nyumbani Tanzania kweli kabisa. Mbali na hilo kwenye Tv za hapa haliongelewi na kutiliwa umakini wowote...hivi kweli kweli hivi? Angekuwa mtu mweusi kafanya hivi....kwasasa tungekuwa tunasakwa sana watu wote weusi na kurudishwa makwetu, bila sababu yoyote....sababu tu mtu mweusi kafanya kitendo kama hiki, lakini kimya...wanaliongea lakini sio ki hivyo sana. Nilitaka kuwa raia wa Italy...lakini nimeghaili kabisa.

Comment by Dixon Kaishozi on December 15, 2011 at 8:49

Hii ndiyo Tiziiiiiii bwana.. nilipelekwa kituoni kwa kumuuliza askari nionyeshe kitambulisho kabla hujanikamata!! hapo ndipo nilipozua balaaa kabisaaa.. kwamba najidai mjuaji.. kidogo nilale selo!!!

Comment by Gratious Kimberly on December 15, 2011 at 5:13

Chibiriti....hiyo ndo picha ya kwenu ya maiti tena wote waafrika... nakuja huko kuchimbua mizizi!!...soo sad!!

Comment by Gratious Kimberly on December 15, 2011 at 5:05

Nilikuchokoza kujua kaka.....mimi mwandishi kaka na kuchokoza ni kazi yangu......Kweli habari hazifanani na hapa...nilitaka kujua unasemaje kwa hilo!!!.... Ila hiyo ya kwenu imeniuma saaana kupita kiasi kaka.....pamoko broooooo!!!!!

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on December 15, 2011 at 4:34

@ Gratious  = Huyo Jamaa alikuwa mbaguzi wa rangi tu, hakutaka kuona weusi katika nchi yake ya Italy, hivyo kuchukua uamzi wa kuwamaliza weusi na yeye mwenyewe kujimaliza, mara nyingi akili za watu hawa huwa sio zima kabisa.....haihusiani kabisa na hii story ya hapa, ya Polisi kupiga raia wasio na hatia na wala haifanani kabisa na hili tunalo liongelea hapa sasa.

Comment by Gratious Kimberly on December 15, 2011 at 3:22

Kweli Chibiriti......Ila nawe usisahau kwamba jana au tuseme juzi huko kwenu kuna mtu amekoki bundukuki na  kuua wasenegali 3 na wengine 5 mahututi hospitali....ebu tupe hiyo ishu maana ililenga watu weusi!!!!!!!!!!!!!!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*