Tulonge

Ama hakika hii ndio tanzania tunayosema inaamani na kuheshimu haki za raia,ebu angalia hawa askari wakimsurubu kijana huyu ambaye si kibaka bali ni raia mwema tu ,lkn kwasabau wao wanazozijua wakampa…

Ama hakika hii ndio tanzania tunayosema inaamani na kuheshimu haki za raia,ebu angalia hawa askari wakimsurubu kijana huyu ambaye si kibaka bali ni raia mwema tu ,lkn kwasabau wao wanazozijua wakampa kosa la kuwakimbia na pikipiki wakati wakimsimamisha barabarani,lkn si kweli kijana huyu ni muuza maji na juice kwenye kituo cha basi,hata ilo pikipiki hajui.

Lkn ndio hivyo wameshaamua kutoa kichapo hicho,sasa tujiulize mimi na wewe mwanatulonge kuna haki hapa  na hiyoo amani wanayohubili kila kukicha hiko wapi.

Inasikitisha kuona mtanzania akinyanyaswa kwa kosa ambalo hakufanya bali amefananishwa tu na mwingine.Ni wangapi wameonewa,wamenyanganywa mali na wana usalama wa bongo,binafsi kikufurahishwa na nimeumizwa na kitendo hiki.

Views: 479

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on December 15, 2011 at 0:03

Hawa Polisi wangekuwa huku Ulaya....sasahivi wapo gerezani kwa kesi kubwa, na faini kubwa sana...mambo ya kupiga piga watu ovyo ovyo tu....sijui tutakuja kuelimika lini? Sijui viongozi wetu hawaoni haya? au ndo makusudi tu! Mimi ningependa sana siku moja nimpelekee mkuu wa Polisi na kumweleza manyanyaso ya raia....walivyo washenzi anaweza kukuweka ndani kabisa. Nikifikiria mambo haya? hapo tu! naghaili kabisa kurudi hata Bongo. Maana wenzetu wanatii sana raia....Trafiki tu wa hapa wakinisimamisha barabarani na gari, kitu cha kwanza wananipigia saluti kwa heshima zote, wanasalimia halafu ndo maswali yanafuata, nilishangaa sana mara ya kwanza...lakini kumbe ndo mazoea yao ya kuheshimi raia. Hivi kanini sisi tusiweze?

Comment by Alfan Mlali on December 14, 2011 at 16:09
Mimi ninachojua Polisi anatakiwa kulinda usalama wa raia na sio kupiga raia hata kama kweli kafanya kosa.Walipaswa kumkamata na kumpeleka kituoni wakamuhoji wajue kisa cha kuwakimbia na kama ni yeye ama siye!!! Kwa kweli inabidi watanzania tufike sehemu tuseme sasa basi tukiona mwenzetu ananyanyaswa na polisi tuchukue hatua za kuingilia na kumtetea mwenzetu..Huwezi jua lini yatakukuta na wewe ukafananishwa na jambazi sugu wakaishia kukupiga risasi bila kupewa nafasi ya kujitetea!
Comment by Mama Malaika on December 14, 2011 at 15:43

Jamani nyumbani kuna uonevu kila kiona... hao wananchi wanaoangalia wakiamua kumtolea huyo police uvivu si atashika adabu yake.

Hii itafikia kama huyu mama wa Tulonge aliyeamua kuchukua sheria mkononi dhidi ya mapolisi

 

http://tulonge.com/photo/polisi-apewa-kichapo-na-mwanamama?context=...

Comment by Tulonge on December 14, 2011 at 14:12

Mkuu Jemedari Tanzania hakuna amani ila kuna ukimya. Hao polisi ndiyo hawajui kabisa mipaka ya kazi yao, wadadhani kupiga raia ni kazi yao.

Comment by Gratious Kimberly on December 14, 2011 at 13:33

Kweli  mkuu hii ni noma...yaani tena hawa askari wanatakiwa wapewe semina kali kuhusu haki za rahia jamaani. Alafu hao raia hapo pembeni wanaona ni sawa bila kjua kwamba kesho inaweza kuwa zamu yao. inatia hasira mazee!!

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*