Tulonge

Admin wa tulonge akabidhiwa zawadi zake na Msanii bora wa hiphop Tanzania, Kala Jeremiah

Kushoto ni Admin wa tulonge.com(Dismas) akikabidhiwa zawadi zake na Kala Jeremiah

Mnamo tarehe 28 Juni 2013 msanii bora wa Muziki wa HipHop Tanzania Kala Jeremiah alitangaza shindano kupitia ukurasa wake wa Facebook. Alitaka wadau waupige picha ukurasa wake wa facebook siku ambayo utafikisha 'likes' 44,444. Mdau wa kwanza kupiga picha hiyo na kutumtumia kwenye 'inbox' yake ndiye mshindi.

Bahati nzuri Admin wa tulonge.com (Dismas Hiza) ndiye aliyebahatika kuwa wa kwanza kutuma picha hiyo na kujishindia sh. 100,000 pamoja na 'Audio Album'  ya msanii huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Mlimani City, DSM.

Stori zikiendelea baada ya kutia changu mfukoni teh teh teh

 

Picha ya ukurasa huo ilionekana hivi:-

Views: 1062

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on August 24, 2013 at 18:10

ha haaa haaaa.... Dismas wapenda vya bure weye, angalia wachaga hao wasije kupiga fine ukajikuta wauza hadi godoro na kitanda. Ha haa haa haaa.....

Comment by Tulonge on August 1, 2013 at 14:06

Manka hapo sijanuna, ndivyo nilivyo teh teh teh. Ishu za mahari nimeamua kuachana nayo. Kwa vyovyote siwezi timiza kiasi mkitakacho. Nimeamua kutumia njia mbadala  ili nimpate mdogo wako. Next week naenda Tanga kwa Babu akanifanyie mavituzi. Nikitoka huko mdogo wako ataanza kung'ang'ania kuwa na mimi tena bila kutoa mahari teh teh teh

Comment by manka on August 1, 2013 at 13:59

HONGERA ADMIN, LAKINI MBONA UMENUNIA PESA!! TEHEE. MAHARI UMEFIKISHA SHILINGI NGAPI VILE?

Comment by Tulonge on August 1, 2013 at 7:04

Mama si nilikwambia zote ziliishia pale pale Mlimani City. Nilipokabidhiwa tu nikazama Shoprite, nilipotoka nilikua na Sh. 500 tu ya nauli teh teh teh

Comment by Mama Malaika on July 31, 2013 at 17:21
Ila Dismas itabidi unilipe deni la langu la mwaka majuzi maana kila siku wanipiga hadithi, haya leo mkwanja umeuanika hadharani huna cha kuongopa. Teh teh teh...
Comment by ANGELA JULIUS on July 30, 2013 at 16:15

duh hongera watu wanaolala mtandao wazi utawajua tu ha ha ha sasa nitakutafuta nikukope hata kidogo

Comment by Tulonge on July 30, 2013 at 12:28

Teh teh teh Pa1 sana Gratious

Comment by Gratious Kimberly on July 30, 2013 at 0:20

Shoprite tena...kwani kina vibua huko siku hizi?   teh teh... hongera mkuu...inaelekea siku hiyo ulikesha hapo kitengo...haaa.  inaelekea alizaliwa tarehe 4 mwezi wa 4...ila mwaka.....wa babu yake...haaa

Wakilisha kamanda!!

Comment by Tulonge on July 29, 2013 at 17:14

Teh teh teh Kunambi imekula kwako. Kwa nini usingetuma wewe?

Comment by KUNAMBI Jr on July 29, 2013 at 16:14

Ebhana nipe changu kabisaaaaaa kabla sijakinukisha maana me ndo nlokushtua utume ule ukurusa,ukidhulumu najua ntakupatia wapi

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*