Tulonge

Afrika Kusini:Takribani watu 40 wafukiwa baada ya jengo kuporomoka

Wengi wa waliofukiwa wanaaminika kuwa wajenzi

Takriban watu 40 wamekwama kwenye vifusi baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.

Inaarifiwa watu 30 wameweza kuokolewa na wengine wawili kuthibitishwa kufariki.

Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.

“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.

Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.

Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.

BBC Swahili

Views: 181

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on November 20, 2013 at 0:09
Haya matukio ya majengo kuporomoka yamezidi, local authorities yapasa wawe wakali kusimami ili kupunguza athari hasa vifo na majeruhi.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*