Tulonge

Aki huyooooo katika Jiji la Gharam la 'Abu Dhabi' akiwa na mkewe

WIKI chache baada ya kufunga ndoa na mkewe, msanii wa Nigeria, Aki, amekwenda Abu Dhabi kula fungate.Abu Dhabi ni mji maarufu na wenye maisha ghali katika nchi za Falme za Kiarabu.

Msanii huyo ambaye alioa kwa siri Ijumaa ya Desemba Pili mwaka jana, fungate yake ililazimika kusubiri kwa muda kutokana na taratibu za uhamiaji pamoja na matakwa ya washauri wake wa karibu.

Inadaiwa msanii huyo atakaa Abu Dhabi wiki mbili kabla ya kwenda kwenye mji mmoja maarufu Barani Ulaya ambao bado haujawekwa bayana.

Lakini hatafanya kazi mpya mpaka mwezi Aprili kutokana na ratiba zake na shughuli za kijamii.

Habari kwa hisani kubwa ya: Mwanasporti.co.tz

Views: 629

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MARTHA MSHANGA on January 31, 2012 at 8:51
Hongera sana Aki,sasa twamsubiri Ukwa.
Comment by manka on January 26, 2012 at 9:48

raha jipeni wenyewe wandugu, maisha yenyewe hay mafupi, na hongereni kwa hataua ya busara(kufunga ndoa). Chalii kwani paris hapaendeki bila kujua kifrench?

Comment by ILYA on January 25, 2012 at 17:34

Hahahaha, kaka dism kweli umenena ,maisha yenyewe haya mafupi ukipata kijichance kama hicho katumie raha za duniani madam hujachukua cha mtu.Aki huyu ananikumbusha ndoto yangu iliyoota mbawa ya kwenda kula maraha huko maeneo ya Jiji la Paris kwa wajanja.

Kilichosababisha ndoto isitimie ni tatizo la Lugha ya kifaransa maana nasikia ili uweze kukitamka vizuri inabidi ung'oe meno mawili yale ya kusaga nyama ya juu ya nachini ,ndio utaweza kuzungumza na kueleweka hususan ikiwa wewe si mwenyeji wa Lugha yenyewe.

Kwani mimi ni mpenzi wa Nyama choma nikaona hiyo safari si iwezi maana itanilazimu kupoteza meno  bure.

Comment by ANGELA JULIUS on January 25, 2012 at 15:02

HONGERENI SANA NAWATAKIA MAISHA YENYE FURAHA NA AMANI

Comment by Bonielly on January 25, 2012 at 11:19
upe raha moyo wako pale unapohitaji na unapokuwa na uhakika na maisha yako, hongera aki, ni mmoja wa wanasanaa ninaowakubali yeye na pacha wake,
Comment by Tulonge on January 25, 2012 at 7:08

Nimeipenda hii,kateseni kwa raha zenu.Maisha yenyewe mafupi haya.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*