Tulonge

Albino wauawa kwa mbinu mpya: Kufunga nao ndoa

Walemavu wa ngozi nchini Tanzania (albino) wamesema kumeibuka mbinu mpya zinazotumiwa na makundi ya watu wanaotumia kigezo cha kufunga ndoa na watu wa jamii hiyo na baadaye hutekeleza azma yao ya kuwaua na kukata viungo vyao.

Kauli hiyo imetolewa na chama cha maalibino nchini Tanzania wakati walipokutana na waandishi wa habari kuelezea hali mpya ya wasiwasi inayowaandama watu wenye ulemavu wa ngozi nchini humo.

Huku wakielezea kuzorota kwa ulinzi na usalama, jamii hii ya walemavu wa ngozi imesema kuwa serikali haijachukua hatua madhubuti kakabiliana na wimbi la matukio hayo ya kikatili ambayo pia yanahusishwa na imani za kishirikina.

Wale wanaoamini nguvu za kishirikina wamekuwa wakiviwinda viungo vya walemavu wa ngozi katika kile kinachoaminika kuwa viungo hivyo vina nyota muhimu inayoweza kuwasaidia watu hao kupata utajiri wa mali.

Tangu kuzukwa kwa imani hiyo, mamia ya watu wenye ulemavu wa ngozi wamepoteza maisha wengine wakisababishwa ulemavu wa viungo na wengine kupoteza ndugu na familia zao.

Wakati matukio ya uvamizi na mashambulizi yakipungua kiasi lakini kumeibuka mbinu mpya ambayo hutumiwa na wajanja wachache kuwarubuni wale wenye ulemavu wa ngozi kwa minajili ya kufunga nao ndoa lakini baadaye ndoa hiyo hugeuka shubiri.

Wachambuzi wa mambo ya kijamii wanasema kuwa serikali bado haijapiga hatua kubwa kuwahakikishia amani watu wenye ulemavu wa ngozi na pia huduma zinazotolewa kwao bado ni za kiwango cha chini.

Imeripotiwa na George Njogopa, VOA, Dar es Salaam.

Views: 403

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by tulamvone mwenda on January 16, 2013 at 7:08

he jamani makubwa

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*