Hivyo ndivyo shabiki Steve alivyo watukana wachezaji Ashley Cole na Ashley Young wa timu ya Soka ya England kupitia mtandao wa kijamii (tweeter) baada ya kukosa penati katika mechi ya robo fainali ambapo England walitolewa na Italy kwa mikwaju ya penati. Shabiki huyo amekamatwa na polisi.
Itakumbukwa mwanafunzi Leam Stacey alihukumiwa kifungo cha siku 56 baada ya kuonesha ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa Bolton Wanderers Fabrice Muamba kupitia tweeter.
Ashley Young (shoto) na Ashley Cole baada ya kukosa penati siku ya mechi yao na Italy.
Add a Comment
Ni kweli kama anavyosema dadaangu Mama Malaika, ni watu walio na low education profile au mlevi ndio wenye tabia hizi.
Ulaya mashariki ndio usiseme....!!!
Kila mahali pana ubaguzi, ukiishi ughaibuni kwa muda mrefu utakuwa kama wimbo wa kumlaza mtoto" zum zum zum nyuki lia weeee....!" .
Kila corner....si nyani tu utaitwa bilinganya, lami, mkaa au kitu chochote kinachofana na weusi.
Dismas .... karne hii ya 21 bado wapo wenye kutuona tunafanana na nyani kama huyu shabiki. Na kwa kisiwa cha Uingereza karibu wote walio na tabia/kasumba hii unakuta elimu is not reachable, (wana elimu duni), wengi wametoka kwenye low class families na hawajapata exposure. Hukuti mtu toka middle class au higher class ana tabia hii, na iwapo utasikia basi ni wachache sana.
Huyu hana akili kabisa. Nampa pole kwani tayari kapewa criminal record na kaingizwa kwenye database. Siku anakataliwa maombi ya professional job sababu ya criminal record ndio akili itamfunguka.
Na kina Ashley wakirudishwa Africa mwenye kuathirika ni yeye na uchumi wa nchi yake (UK) kwani kipato chao kikubwa na wanalipa kodi kubwa (50%).
watuletee tu watu wetu sisi tunawakubali sana tena wapo juu.
Hivi ni kweli hawa jamaa wanatuona cc tumefanana na nyani? Duuh
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge