Tulonge

Aliyeghushi saini ya Waziri Mkuu, Pnda asomewa apandishwa kizimbani

Imeandikwa na Happiness Katabazi, Tanzania Daima — MFANYABIASHARA Amadi Ally Popi (35), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikakabiliwa na makosa mawili likiwemo la kughushi barua inayoonyesha imeandikwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Inspekta wa Polisi Hamis Said mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alilitaja kosa la kwanza linalomkabili Popi ni la kughushi kinyume na kifungu cha 333,335(a) na 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Inspekta Said alidai kuwa tarehe na siku isiyofahamika ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa nia ya
kudanganya Popi alighushi barua yenye kumbukumbu Na,DA21/3078/01A/142 ya Desemba 3 mwaka 2012 akijaribu kuonyesha kuwa barua hiyo ni halali na ilikuwa imeandikwa na kusainiwa na Waziri Mkuu Pinda.

Said alilitaja kosa la pili kuwa ni la kutengeneza nyaraka ya serikali bila ya kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kosa ambalo ni kinyume cha kifungu cha 346(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, ambapo tarehe na siku isiyofahamika ndani ya jiji la Dar es Salaam, Popi bila ya kuwa na mamlaka yoyote alitengeneza barua hiyo na kuisani na kisha alimpatia barua hiyo Islamu Mohammed Mtila akijaribu kuonyesha barua hiyo imetoka katika ofisi ya waziri Mkuu na imesainiwa na Waziri Mkuu Pinda.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alikanusha mashitaka yote na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wanaofanyakazi serikali au kwenye taasisi zinazofahamika ambapo watasaini bondi ya Sh. milioni 10 na mmoja katika wadhamini hapo atawasilisha mahakamani hati ya mali isiyoamishika yenye thamani hiyo, masharti ambayo yalishindwa kutekelezwa na mshitakiwa huyo na hivyo hakimu Lema aliamuru mshitakiwa apelekwe rumande hadi Septemba 5 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa na upepelezi wa shauri hiyo haujakamilika.

Views: 358

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on August 25, 2013 at 17:20
Mr Amadi Popi thinks he's smart, yet gets it all wrong and falls off the rails with a thud.
Comment by Samwel Mnubi Masatu on August 24, 2013 at 1:00

kanyee ndoo

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*