Taarifa zinasema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu, Mhe. Clement Mabina ameuwawa na wananchi wenye hasira kwa kupigwa na mawe na silaha za jadi mwendo wa saa 2 asubuhi katika kijiji cha Kanyama.
Imeelezwa kuwa chanzo cha shambulio lililomuua Mabina inatokana na ugomvi wa ardhi ambapo kesi ya eneo hilo ilikuwa ikiendelea mahakamani, lakini mchana wa leo, marehemu Mabina alionekana akipanda miti na kuweka mawe ya msingi katika eneo lenye ugomvi na wananchi walipomhoji kuhusu kibali cha mahakama cha kufanya hivyo, inaripotiwa kuwa aliwatolea lugha chafu na kuwatisha kwa bunduki ambapo alifyatua risasi ili kuwatawanya.
Inaripotiwa kuwa moja ya risasi iliyofyatuka ilimpata mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kumsababishia mauti. Baada ya risasi kuisha, ndipo wananchi walimzingira, wakamvamia na kumpiga kwa silaha mbalimbali ikiwemo mawe, mishale, mikuki na mapanga hadi kumsababishia mauti.
Kabla ya kurejea CCM, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.
Mabina pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.
Mwaka 2012 akiwa CCM, aligombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama ngazi ya Mkoa wa Mwanza lakini alishindwa na aliyewahi kuwa Waziri na Mbunge wa Ilemela Dk Antony Diallo.
Taarifa zaidi zitapatikana kwenye vyombo rasmi vya habari hapo baadaye.
Maelezo na wavuti.com
Add a Comment
Pole sana Mama Malaika.. ila wanacho kitafuta ni kama cha huyu bwana.. Watu Wakisha choka kifuatacho ndiyo kama hicho!!! Pole sana, vyote ni vyakupita. Aridhi hii tunayopigania mwisho wake itatufukia tu!!!
Siku zote usibishane na nguvu ya umma! Hutowaua wote hata kama silaha ya moto!
Hiyo ndiyo nguvu ya uma!! Alitaka kutumia ubabe matokeo yake ndiyo hayo.. Kaua na yeye kauliwa.. malipo ni hapa hapa duniani. Kwa upande wangu siwezi shiriki kutoa mtu roho.. ila simuonei huruma hata!! Hawa jamaa wanaona nchi ni yao.. cccm!!! NAAMINI SIKU WANANCHI WAKICHOKA - HATA MJE NA VIFARU.. HIKI NDICHO KITAKACHO TOKEA!!!!
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge