Kwaya ya kisabato toka Kigali Rwanda inatarajia kufanya ziara Bongo na kutangaza injili ya Bwana katika ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya tarehe 4/12/2011 kuanzia saa 7 mchana. Kiingilio ni sh 20,000 (VIP), SH 10,000/5,000 (Kawaida). Kwaya hiyo ambayo imetamba na nyimbo zake nzuri ikiwemo kwetu pazuri imekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake ,ona hapo chini.
Tazama moja kati ya nyimbo zao zinazotamba hadi sasa http://tulonge.com/video/christ-ambassadors-choir-kwetu-pazuri
Add a Comment
Safi sana,tunawasubiri kwa hamu.
Wengine itabidi tuanze kuabudu dini za mababu zetu hazina kokolo. Kule alikotoka bibi yangu mzaa mama hadi leo kuna nduguze hawajui ukristo wala uislamu bali wana abudu dini ya asili na huwaambii kitu. Ha haa haaa
Mama siku hizi ni fweza kwa kwenda mbele, siku hizi hata wachungaji wanatumia muda mwingi kuhubiri kuhusu sadaka.
Ama kweli dini siku hizi imegeuka biashara maana kila kitu kihusucho dini kimekuwa ni hela hela hela, hadi kwenda kusikiliza Gospel Choir toka nje ya nchi ni hela. Miaka ya nyuma zilizokuwa zinakuja bongo zaimba bureee bila viingilio hasa kipindi cha wahubiri kina Moses Kulola.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge