Tulonge

Amnajisi mtoto kwa ngono ya mdomoni kwa hadaa ya kumpa mwanasesere

Habari ifuatayo imeandikwa Walter Mguluchuma, Mpanda, Katavi via HabariMseto blog — Fundi aiskeli mmoja mkaazi wa mtaa wa Nsemlwa, wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi, Athumani Mussa (54) amefikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumlawiti (kunajisi) mdomoni mtoto msichana (4) baada ya kumdanganya kumpatia mdoli wa kuchezea.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka mkaguzi wa msaidizi wa polisi Razalo Masembo mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa.

Mwendesha mashitaka aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa Athumani Musa alitenda kosa hilo Julai 24
mwaka huu majira ya saa 12 jioni nyumbani kwake katika mtaa wa Nsemlwa mjini hapa.

Mtuhumiwa anadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio alimwona mtoto huyo akiwa na wenzake wakicheza barabarani karibu na nyumbani kwake ndipo alipomwita mtoto huyo na kumwambia amfuate nyumbani kwake ili akampe mdoli wa kuchezea. Mara baada ya mtoto huyo kuingia ndani, mtuhumiwa alianza kumnajisi mtoto huyo mdomoni huku akiwaamekaa kwenye kochi lake sebuleni.

Ilidaiwa kuwa licha ya mtoto huyo kupiga mayowe ya kuomba msaada, mtuhumiwa hakujali mayowe ya mtoto huyo bali aliendelea na shughuli yake hadi hapo alipomaliza haja yake.

Mwendesha mashitaka alidai kuwa mtoto huyo alipotoka nyumbani kwa mtuhumiwa alielekea nyumbani kwa mama yake huku akilia kwa sauti kubwa, hali iliyosababisha watoto wenzake wamfuate kwa nyuma.

Masembo alieleza mara baada ya kufika kwa mama yake na kuulizwa analia nini, mtoto huyo alitema mdomoni mbele ya mama yake shahawa akimweleza mama yake alichofanyiwa na fundi baiskeli, Musa.

Mama wa mtoto huyo aliangua kilio na kufanya majirani wakusaniyike na ndipo alipowasimulia mkasa huo.

Majirani hao walipochukua jukumu la kwenda kumkamata mtuhumiwa wakiwa wanaongozwa na mtoto huyo ambaye alikataa kuingia ndani ya nyumba ya mtuhumiwa kwa kudai anaogopa kunajisiwa tena na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa Athumani Musa alikana shitaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa aliamuru mshitakiwa apelekwe rumande hadi Septemba 2 kesi yake itakaposikilizwa.

via:wavuti.com

Views: 931

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on September 19, 2013 at 17:24

MBWA HUYO

Comment by MGAO SIAMINI,P on August 24, 2013 at 11:20

mshenzi!

Comment by Geoffrey Masai on August 24, 2013 at 11:02

haya mambo zamani hayakuwepo kabisa, utanda wazi umeleta majanga hasa Tanzania, kila siku matukio ya ajabu ajabu tu.

Comment by ANGELA JULIUS on August 24, 2013 at 9:19

KISHERIA HUYU MPUMBAVU NI KIFUNGO CHA MAISHA KWANI AMEMNAJISI MTOTO CHINI YA MIAKA 12.

NAYE AENDE AKANYONYE MABORO YA WENZIE NA KULAWITIWA TENA MALIPO HAPA HAPA NINA UHAKIKA ANACHOENDA KUFANYIWA HUKO NI ZAIDI YA ALIVOMFANYA MALAIKA WA WATU. JAMAA HILI NI CHAWI KABISA HAFAI KWENYE JAMII.

Comment by Samwel Mnubi Masatu on August 24, 2013 at 1:06

mmmmm! jaman  dunia bas

Comment by Mama Malaika on August 23, 2013 at 21:19
Hii balaa.... Ningekuwa mama wa huyo mtoto kwa hahika ningemuinglia huyo bwana ndani mwake na panga kuumata uume wake niuweke mdomoni kwake tuone.. Nasikia hasira sana, mtoto wa miaka 4 kumfanyia hivyo. Khaaa...
Comment by Omar on August 23, 2013 at 17:52

Watu kama hawa ni kupewa adhabu kali mno ili uwe mfano kwa wengine,wewe waanawake wa umri wako wapo kibao tena hata ukitaka zaidi ya umri wako unaenda kumfanyia kitendo cha kishenzi mtoto wa mwenzio, wapo dada poa kibao tena wanakopesha! unashindwa kwenda kuongea nao unaenda kuharibu New Generation.Umenitia hasira saana tena saana! dawa yako wewe ni kufungwa miaka 30  tu tena na kazi ngumu kabisa huwezi kuharibu kizazi kipya kabisa shwaini weee! kakope wapo wanakopesha mbona! ahhh kweli nimeamini hakuna kabila la watu wanaitwa washenzi ila mtu ni vitendo vyako tu ndivyo vitakufanya uitwe mshenzi!

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*