Tulonge

Aongoza kundi kumbaka na kumlawiti mzazi mwenza hadi akafa

JESHI la Polisi mkoani Manyara, linamshikiliwa mkazi wa Kijiji cha Gijachameda, Wilaya ya Babati, Bw. John Barandi (35), kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzazi mwenzake Mwanaisha Iddi (25), baada ya kumbaka na kumlawiti.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Akili Mpwapwa, alisema tukio hilo limetokea Januari 10 mwaka huu, saa 11 jioni, eneo la Mrara wilayani humo.

Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa mjini Babati alimpigia simu mzazi mwenzake ambaye inadaiwa walizaa naye watoto wawili ili wakutane na kwenda kufanya mapenzi.

“Marehemu alikwenda kwa mzazi mwenzake na kwenda kufanya naye mapenzi katika korongo la maji lilipo Mrara, baadaye huyu mtuhumiwa alitaka kumwingilia mwenzake kinyume na maumbile lakini marehemu alikataa. Ghafla kundi la wanaume lilitokea upande mwingine wa korongo ambao walimlazimisha marehemu akubali... wote walimkamata huyu marehemu na kuanza kumwingilia mmoja mmoja kinyume na maumbile hadi kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema.

Aliongeza kuwa, wapita njia walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa uchi nguo zake zikiwa pembeni akiwa ameonekana ambapo hadi sasa, jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina.

“Hadi sasa tunamshukia mtuhumiwa pekee ambaye alikutwa kwa mganga wa kienyeji akipewa dawa ya kumzuia asikamatwe na polisi, atafikishwa mahakamani wakati wowote,” alisema.


Habari imeandikwa na Jamillah Daffo, MAJIRA, Babati.

Views: 704

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 18, 2013 at 11:38

kweli kaka D VICHAA ni wengi kitaa sema kila mtu na kichaa chake,kawadhalilisha watoto wake,na mpenzi wake ambaye bado alimuamini akaenda kumsikiliza watu hawa wanatakiwa kunyongwa nyie mnasema sheria hiyo ifutwe? haya mchagulieni adhabu huyu jamaa.

Comment by Dixon Kaishozi on January 17, 2013 at 8:37

Yani huyu jamaa nimeshindwa kumuelewa kabisa......

Comment by Mama Malaika on January 16, 2013 at 16:42

Na huyu bwana hamnazo kabisa. Haya kaua mzazi mwenzie aliyekuwa akilea watoto wake, bado anakwenda kwa mganga wa kienyeji kupewa dawa ili asishikwe. Nani aliyemwambia kuwa unapo ua unaweza jificha?? Ukijificha duniani bado kwa Mungu hujifichi, anakuona na atakuhukumu.

Comment by william massawe on January 16, 2013 at 15:49

du!!!! ubongo wa mjusi!!!!!!!!!!!

Comment by Christer on January 16, 2013 at 12:43

Mijanaume mingine bwana, hivi unampeleka mzazi mwenzako porini ili mkazini kweli? huna nyumba? Muuaji huyo anyongwe!!

Comment by kabegulahamza on January 16, 2013 at 10:22
huyu kweli chizi.
Comment by tulamvone mwenda on January 16, 2013 at 7:14

jamani alaaniwe huyu baba atawaambia nn watoto wake 2 waliobaki, R.I.P Mwanaisha

Comment by Tulonge on January 15, 2013 at 21:01

Ndomaana mimi huwa nasema kuna vichaa wengi sana bado tupo nao mtaani

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*